NEW YORK, Marekani
Imebainika kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa
makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya ya
binadamu.
Wataalamu wa mambo wanadai kwamba pamoja na kuongeza ukubwa
wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi ya makalio katika
mpangilio usio sahihi.
Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa
wa ugonjwa wa saratani.
Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke aliyeongeza
makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na
matumizi ya madawa hayo huku akisema : "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa
makalio yangu".
Anaongeza: "Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi. Nadhani
kuna ulazima wa kuyaondoa haya makalio yangu yote kwa sasa." alisikika
akisema.
Mpaka kufikia jana video hiyo ambayo pia iliwekwa katika
mtandao wa kijamii wa Facebook tayari ulikuwa umependezwa na watu 278,000
wanaotembelea huku ikiwa imehamishwa na watu zaidi ya 430,000 wakipeleka katika
kurasa zao.
Mtumiaji mmoja wa mtandao huo kutoka nchini Marekani Donna
Wright-Levy, alichangia akisema: "Mimi hupendelea kwenda maeneo kadhaa ambako
hutengenezwa shepu yangu kwa madawa haya sasa nina ulazima wa kwenda kupima
saratani".
Ni vigumu kuthibitisha mwanamke huyu alitumia kliniki gani
wakati alipofanyiwa uongezwaji wa ukubwa wa makalio yake miaka miwili
iliyopita.
Lakini mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya upasuaji ya
BAAPS Aurora nchini Uingereza Adrian Richards, ambaye pia ni mshauri wa upasuaji
anaamini kuwa mwanamke huyo alifanyiwa marekebisho ya makalio yake kwa dawa za
silicone.
Alisema tatizo hutokea wakati nyama ya makalio inaposhindwa
kuulinda vema mwili na kuwa imara katika nyama na mifupa na hivyo madhara huanza
kutokea juu ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya nyama na baadaye mfupa.
Ni matatizo ambayo ni ya kawaida kumfika mtumiaji ya dawa
za kuongeza ukubwa wa maumbile iwe ni matiti ay makalio. Ni lazima itokee baada
ya muda maana kama kitu kilipulizwa na upepo ina maana wakati wake ukiisha
kitarudi kama awali.
"Huyu mwanamke aliyaongeza makalio yake kwa nyuma na kwa
juu zaidi hivyo tayari madhara yake yamekuwa ni makubwa kwa maana hakufanya
upasuaji bali alitumia njia za mkato za silicone, " alisema
Alisema ni lazima anapata maumivu makali, lakini
alipendekeza kuwa ni vema kama makalio hayo yangeondolewa kabisa ili kuzuia
maambukizi kuendelea.
Uongezwaji wa makalio ni jambo lililoshamiri mno Amerika ya
Kusini ambapo ukubwa wa makalio unapimwa kama kigezo kimojawapo katika
ngono.
Katika miaka ya karibuni, upasuaji na uongezwaji wa makalio
ni kati ya mambo yaliyopigwa vita huku wanawake wengi wakionywa sana ambapo
idadi kubwa ya watu maarufu pamoja na wengine wamekufa kufuatia huduma
hii.
Mwezi Aprili mwaka jana, mama wa watoto watatu mwenye umri
wa miaka 42 alifariki wakati akifanyiwa upasuaji wa kuongeza ukubwa wa makalio
yake katika kliniki moja huko Las Vegas.
Desemba 2009, aliyekuwa Miss Argentina alifariki dunia
wakati akijitahidi kufanyiwa upasuaji wa kuongeza ukubwa wa makalio yake.
Solange Magnano, 38, aliwahishwa hospitalini kwa ajili ya
kufanyiwa matibabu baada ya kuzidiwa katika kliniki ya oparesheni ya vipodozi
kwa kushindwa kupumua.
Habari iliyosambaa duniani mwaka 2011 ni kuhusiana na April
Brown, raia wa Marekani ambaye alikuwa mwanamitindo, kutokana na tamaa yake ya
kuwa na makalio makubwa, alijikuta akikatwa miguu na mikono baada ya kuchoma
sindano zenye dawa za kumuwezesha kuwa na umbile hilo.
Akizungumza kwa masikitio na mtandao mmoja wa habari za
kijamii, mrembo huyo alisema: “Ni tukio lililoyateteresha maisha yangu. Nilikuwa
na umbile la kawaida tu lakini nikaingiwa na tamaa na kusaka makalio
makubwa.
“Wapo walionishauri nitumie vidonge lakini baadaye
nikaambiwa naweza kupata shepu hiyo kwa kuchoma sindano.
“Nilichoma sindano hizo kwenye zahanati bubu na mwanzoni
niliona mabadiliko kwa kuongezeka lakini baadaye nikaanza kujisikia hali ya
tofauti, nilipokwenda hospitali wakaniambia nimepata infections
(maambukizi).
“Kadiri siku zilivyozidi kwenda, hali yangu nayo ilizidi
kuwa mbaya na nilivyokwenda kwa daktari aliniambia kwa maambukizi niliyopata
kutokana na kuchomwa sindano yenye silkoni inayotumika viwandani, ilikuwa lazima
nikatwe miguu na mikono.
“Sikuwa na jinsi, ilibidi nikubaliane na ushauri wao na
ndipo nilipopata kilema hiki,” anasema April ambaye sasa anaendesha kampeni ya
kuwaelimisha wanawake wenzake juu ya madhara ya kutumia madawa ya kuongeza
makalio.
Hali ikoje nchini?
Kwa hapa nchini baadhi ya mastaa na wengineo wanadaiwa
kutumia dawa hizo maarufu kama za
Kichina kwa lengo la kuongeza makalio na matiti yao.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilishawahi kuteketeza
dawa nyingi za kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume, dawa za Kichina za kuongeza
makalio, kurudisha bikira, kukuza matiti, kuongeza hips, kukuza uume na kahawa
ambayo hutumika kuongeza hamasa kwa wanawake.
Wafanyabiashara wengi
wamekuwa hawatumii misingi ya utaratibu na kanuni za vyakula dawa na
vipodozi. Dawa za Kichina zinazouzwa kila kona zimekuwa na athari kubwa kwa
maisha ya binadamu na baadhi zimekuwa zikiongeza shinikizo la damu.
Licha ya njia hiyo, pia kuna aina nyingine ya kukuza ukubwa
wa makalio inayotumiwa kwa sasa na wanawake wengi hasa wa mjini si ya kumeza
wala kupaka dawa bali ni ya kuvaa taiti zilizojaladiwa vifaa maalum vilivyotuna
mithili ya makalio.
Mmoja wa wafanyabiashara wa ‘makalio’ hayo
aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sanura, alisema ubunifu huo umekuja kufuatia
utafiti kuonesha kuwa baadhi ya wanawake wanatamani kuwa na makalio makubwa ila
wanaogopa kutumia dawa za Kichina.
“Wanawake wengi wanatamani kuwa na makalio makubwa lakini
hawakujaaliwa kuwa nayo, wapo ambao wamefikia hatua ya kutumia zile dawa za
Kichina na ilipobainika zina madhara wameacha.
“Watu wakakaa na kuumiza vichwa, ndipo walipogundua njia
hii ambayo ni salama kwani anachotakiwa kufanya mwanamke ni kununua taiti hizo
ambazo ndani yake kuna kitu chenye shepu ya kalio na hips, akivaa na suruali au
sketi, huonekana amejaaliwa kumbe hamna kitu,” alisema mama huyo mwenye duka
lake la nguo maeneo ya Kariakoo, jijini.
Post a Comment