SEHEMU ya shehena ya madini yaliyoporwa kutoka katika ofisi za kampuni ya
uchimbaji ya Tanzanite One ya nchini Afrika Kusini, imekamatwa ikiwa imefichwa
katika boma moja la Mmasai katika kijiji cha Mererani, mkoa wa Manyara.
Katika tukio hilo pia polisi inawashikilia watuhumiwa zaidi ya 13 kuhusiana na ujambazi huo ambao bado una utata mkubwa kutokana na jinsi ulivyofanyika kiaina.
Chanzo chetu kutoka ndani ya kampuni hiyo kilieleza kuwa tukio la kukamatwa kwa shehena hiyo lilitokea usiku wa kuamkia jana kufuatia msako mkali unaofanywa na makachero kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Manyara, Dar es Salaam na Arusha.
Madini hayo yalikutwa yamehifadhiwa katika nyumba moja ya mfanyabiashara wa kabila la Kimasai ambaye naye inadaiwa alikamatwa, hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa Manyara limekataa kutaja jina lake na majina mengine ya watuhumiwa 12.
Taarifa hizo ambazo zilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa, zilisema kuwa kupatikana kwa shehena hiyo ya madini kunatokana na taarifa kutokana na msako mkali unaoendeshwa na polisi.
“Ni kweli tumefanikiwa kukamata shehena ya madini yaliyoporwa katika ofisi za Tanzanite One pamoja na mtuhumiwa akiwa ameyaficha ndani ya nyumba yake na pia tunawashikilia wengine 12 kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo, lakini tunaendelea na upelelezi,” alisema.
Vyanzo vya habari viliendelea kudokeza kuwa miongoni mwa wanaoshikiliwa ni wafanyakazi saba wa kampuni ya Tanzanite One huku thamani halisi ya kiasi kilichoporwa ikiwa bado haijafahamika.
Katika tukio hilo watuhumiwa walifanikiwa kuingia ndani ya chumba kinachohifadhi madini hayo kwa kukata kipande cha paa la bati na kuingia ndani na kuharibu kamera za CCTV kisha kutekeleza uhalifu wao kwa kutoa madini yaliyokuwa katika kasiki ya kampuni hiyo.
Pia watuhumiwa hao waliweza kuiba madini mengine yaliyokuwa yamehifadhiwa katika madumu na kutokomea nayo kusikojulikana.
Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe, alizungumzia tukio hilo akisema kuwa bado anaamini wahusika watapatikana ili kuondoa shaka iliyopo mbele ya jamii kwamba limefanywa kwa kushirikisha na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo.

CHANZO: TANZANIA DAIMA
Post a Comment