Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa tatu kulia)
akiwasili katika Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha Shelys kilichopo
Mwenge jijini Dar huku akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa
Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ( wa pili kulia), Mkurugenzi wa
Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga
na Wataalamu wa Kitengo cha Mazingira kutoka katika Wizara yake katika muendeleo
wa ziara za kushtukiza Viwandani kukagua mfumo wa mazingira ya maji taka yenye
kemikali katika viwanda hivyo kama unaendana na viwango
vilivyowekwa.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akieleza dhumuni la
ziara yake katika kiwanda hicho kwa Afisa Rasilimali watu wa Kiwanda cha dawa
cha Shelys Bw. Nissa Mwaipiana (kulia).
Mkuu wa Idara ya
Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri na Ujumbe wake.
Mkuu wa Idara ya
Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akimwongoza Mh. Charles
Kitwanga kwenda kukagua sehemu ya kutibu maji taka yenye
kemikali.
Mwendesha Mashine wa
Kiwanda hicho Bw. Patrick Mapunda (mwenye koti) akitoa ufafanuzi Kwa Naibu
Waziri Mh. Charles Kitwanga wa namna wanavyokusanya na kuyatibu maji taka
yanayotokana na uzalishaji kiwanda hapo.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maagizo wa NEMC
baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho kutofikia ubora
unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga(wa pili kulia)
akiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar
Bw. Ernie Van Vreden (kulia) kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho.
Country PAC Manager wa kiwanda hicho Bw. Evans Mlewa (wa pili kushoto)
na kurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact
Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Bw.Ignace Mchallo.
Meneja Uzalishaji wa
Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden akitoa Maelezo
kwa Mh. Kitwanga juu ya Mitambo Mipya ya Kisasa yenye kiwango cha Kimataifa kwa
ajili ya kutibu maji taka katika Kiwanda hicho.
Mh. Kitwanga na Ujumbe
wake ukitizama Bwawa la Samaki linalotumika kufanyia majaribio ya maji taka
ambayo yamekwisha safishwa kwa ajili ya matumizi mengine kiwandani
hapo.
Mh. Charles Kitwanga
(kulia) akitoa maoni yake baada ya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda
cha CocaCola na kuridhishwa na utaratibu unaotumika katika uzalishaji wa bidhaa
zao na mfumo wa kuhifashi maji taka na kuyasafisha kwa njia ya kisasa na kuitaka
kampuni hiyo iwe mfano wa kuigwa na iwe Mwalimu kwa Makampuni
mengine.
Meneja Mkuu wa Kiwanda
cha Soda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios (katikati) akitoa shukrani kwa Mh. Naibu
Waziri na kuahidi kutoa ushirikiano wa kitaalam kwa viwanda vingine juu ya
utunzaji wa maji taka na namna ya kuyasafisha kisasa kuepuka kuharibu Mazingira
na kuongeza kuwa Kampuni ina mkakati kabambe kwa mwaka 2013 kutengeneza ajira
kwa vijana ambapo inakusudia kujenga vituo katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya
vijana kukusanya chupa za plastiki zinazotokana na kiwanda hicho kwa ajili
kuzalishwa upya.
Naibu Waziri Mh.
Charles Kitwanga katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha CocaCola
Bw. Basil Gadzios na Ujumbe wa NEMC na Maafisa wa Wizara
yake.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa pili kushoto)
akiwasili katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli
hiyo iliyopo ufukweni mwa bahari inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja
Mkuu wa Hoteli ya White Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo
Bi. Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa
Hoteli hiyo akifunua chemba inayopitisha maji taka kwa ajili ya kukaguliwa na
jopo la wataalam kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga
hakuridhishwa na jinsi hoteli hiyo inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na
kuagiza timu ya wataalam kutoka NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo
hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli
ya Giraffe Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mh.
Kitwanga (wa pili kushoto) jinsi hoteli hiyo inavyotunza mazingira na namna
inavyodhibit mfumo wake wa maji taka kuhakikisha kwamba haileti
madhara.
Hii ni sehemu iliyoko
pembeni ya Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake hafahamiki ambayo imewekwa uzio
na kufanya bahari kushindwa kupumua vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu
unaodaiwa kutuama mahali hapo tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji
la Dar es Salaam. Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa
faini na kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake
wakiangalia eneo hilo.
Mh. Charles Kitwanga
(kushoto) akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven
Lippinghof baada ya kuwasili hoteli hapo kwa ziara ya kushtukiza kukagua miundo
mbinu ya maji taka kwa hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe za bahari ya
Hindi.
Mh. Charles Kitwanga
akielekea kufanya ukaguzi wakati wa ziara yake ya kutembelea hoteli mbalimbali
za jijini Dar es Salaam zilizopo pembezoni mwa fukwe za bahari ya
Hindi.
Wataalamu kutoka NEMC
na Maafisa wa Wizara wakikagua moja ya chemba za hoteli hiyo zilizounganishwa na
mabomba yanayochuruzisha maji baharini ambapo Hoteli hiyo ilidanganya kwa kusema
kwamba kila chemba hizo zinapojaa wanaita gari maalum la kunyonyea maji taka
hayo kitu ambacho si kweli kwa mujibu wa watalaam wa
NEMC.
Moja ya bomba la maji
taka kutoka katika hoteli hiyo yanayotiririkia
baharini.
Pichani ni Matundu ya
mabomba ya maji machafu yanayotokea Hoteli ya Double Tree By Hilton
yaliyoelekezwa baharini.
Naibu Waziri Mh. Charles
Kitwanga akitoa amri kwa Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira
(Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ambapo ametoa muda wa miezi miwili kwa
uongozi wa Hoteli ya Double Tree kutafuta njia nyingine ya kumwaga maji taka
isiyochafua fukwe na maji ya bahari akisema kuwa yeye si mzungumzaji sana bali
anasimamia vitendo. Mheshimiwa Waziri amemtaka Bwana Mchallo kusimamia
utekelezaji wa zoezi hilo.
Mwanasheria wa NEMC Bw.
Mwanchane Heche akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema watachukua
hatua kuanzia kesho (7 Disemba 2012) kwa kuwa Afya za watu hazisubiri muda hivyo
tunauwezo wa kumfungia biashara yake, kumlipisha faini au vyote kwa pamoja na
tutahakikisha anaacha kumwaga maji taka eneo la
baharini.
Mwanasheria wa NEMC
Bw. Mwanchane Heche akimpa utaratibu wa mamlaka yake hatua itakayochukua Meneja
Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven Lippinghof akimweleza kuwa
japokuwa huduma zao ni bora mfumo wao wa maji taka unahatarisha Afya za Wananchi
na kuharibu Mazingira.
Huu ni muonekano wa
Hotel ya Double Tree By Hilton kwa nyuma Upande wa bahari ambako ndiko wateja
wao wanakopumzika na kupunga upepo mwanana wa baharini kunakomwagwa maji machafu
ya kinyesi.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga ( wa pili kushoto)
akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Coral Beach Hans Heuer (kushoto) ambako
alihitimisha ziara yake.
Mh. Charles Kitwanga na
Ujumbe wake wakikagua miundo mbinu ya eneo la Coral Beach
Hoteli.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maoni yake kwa
Uongozi wa NEMC na kusema kuwa ameridhishwa na hali ya mazingira na utaratibu
unaotumiwa na Hoteli hiyo.
Post a Comment