
Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano, Mhe. Balozi Rajab Gamaha (aliyesimama)
akifungua Mafunzo ya Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Uwazi (OPRAS) kwa Wakurugenzi
na Maafisa wa Wizara yaliyoendeshwa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Bw.
Dushhood Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Neema, Mkufunzi kutoka Utumishi na Bi.
Elizabeth Makyao kutoka Utumishi.

Bi. Neema kutoka Utumishi
akisisitiza jambo kuhusu mafunzo hayo kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara
(hawapo pichani) huku Balozi Gamaha
akisikiliza.

Bi. Elizabeth kutoka
Utumishi akiwasilisha mada kuhusu mfumo huo wa upimaji kazi kwa njia ya uwazi
(OPRAS) kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara (hawapo pichani) huku Bal. Gamaha,
Bw. Mndeme na Bi. Neema wakimsikiliza.

Baadhi ya Wakurugenzi na
Wakuu wa Vitengo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mafunzo
hayo.

Baadhi ya Wakuu wa
Vitengo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki mafunzo
hayo.

Baadhi ya Maafisa kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo ya
OPRAS.

Maafisa wengine wa Mambo
ya Nje wakiendelea na mafunzo ya OPRAS.

Baadhi ya Wakurugenzi na
Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.

Maafisa Waandamizi kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na mafunzo ya
OPRAS.

Sehemu nyingine ya
Watendaji Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mafunzo hayo.Picha
Zote na Habari na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa


Post a Comment