Uganda inaongoza kuwa nchi ya kwanza duniani yenye idadi kubwa ya vijana.
Kwa mujibu wa takwimu za taifa za idadi ya watu za mwaka 2012, zinaonyesha kuwa asilimia 78 ya idadi ya watu nchini Uganda wana umri wa chini ya miaka 30 na asilimia 52 wana umri chini ya miaka 15.
Inaarifiwa kuwa nchini humo kuwa watu milioni 6.5 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 30, idadi ambayo inachangia asilimia 21.3 ya idadi ya watu.
Kizazi cha umri huo kinatarajiwa kuongezeka na kufikia vijana milioni 7.7 ifikapo mwaka 2015.
Aidha ripoti hiyo imeitaka serikali ya Uganda kuwashirikisha vijana katika mipango ya maendeleo ili kupunguza wingi wa vijana tegemezi.
Akiizindua ripoti hiyo Waziri wa Fedha Maria Kiwanuka ametahadharisha kuwa Uganda siku za usoni itakabiliwa na janga la uwiano, iwapo ongezeko la idadi kubwa ya watu haitaendana na huduma bora za kijamii.