Ibrahim Matebu
akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya
kukutanishwa na ndugu zake kufuatia kipindi cha Maisha Plus kumhoji na kuelezea
matatizo yake mara baada ya kutelekezwa na mama yake Hedinesta Kileo kwenye basi
mpakani mwa Tanzania na Kenya, ambapo kijana huyo akiwa bado mchanga aliokotwa
na mama wa Kisomali ambaye alimlea mpaka alipofikisha miaka minne na yeye
akamtelekeza , ndipo alipochukuliwa na serikali ya kenya akalelewa na kusoma
huko.
Ibrahim alirudi nchini kwa
kumfuata rafiki yake hakumtaja jina ambaye inadaiwa ni mkenya wakawa wanaishi
mkoani Arusha, na ndipo alipofanikiwa kuingia katika kuwania nafasi ya kushiriki
katika Shindano la Maisha Plus, hata hivyo hakufanikiwa kupita katika mchujo
huo.
Mama mkubwa wa Ibrahim
alimfananisha Ibrahim na mshindi wa pili wa Maisha Plus Venance Mushi ambaye
ukiangalia kwa kiasi wanafanana, kutokana na historia aliyoitoa Ibrahim jambo
lililompa mashaka kwani mdogo wake Hedinesta aliwahi kuwa na mimba lakini
haikujulikana kilitokea nini mara baada ya kukimbia nyumbani kwao Arusha na
kwenda kwa dada yake huko mpakani mwa kenya na Tanzania ambako inadaiwa
alijifungua na baada ya mwezi mmoja akumtelekeza mtoto huyo, aliyeshika kipaza
sauti ni Emanuel Anderson ndugu yake na Ibrahim
Post a Comment