Waislamu mbali mbali wakiushindikiza mwili wa Marehemu Bi. Zaynab Suleiman (Mama yake Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu) katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya wanafamilia wakiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu, wakisubiri mwili wa mama yao marehemu Bi Zaynab Suleiman kwa ajili ya kumzika katika makaburi ya Mwanakwerekwe. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa CUT Taifa Prof. Ibrahim Lipumba.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu, akichota mchanga kuweka katika kaburi la mama yake marehemu Bi. Zaynab Suleiman baada ya kumzika katika makaburi ya Mwanakwerekwe. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa CUT Taifa Prof. Ibrahim Lipumba.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na baadhi ya waislamu waliohudhuria mazishi ya mama yake Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismali Jussa Ladhu marehemu Bi. Zaynab Suleiman katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Post a Comment