Mama Salma Kikwete na Mke
wa Rais wa Zambia Dk. Christine Kaseba Sata wakimsikiliza Mke wa Rais Mstaafu
wa Afrika Kusini Mama Graca Machel wakati wa hafla ya chakula cha usiku
alichoandaa Rais Jakaya Kikwete kwa heshima ya wajumbe wa Taasisi ya Kimataifa
ya Gavi Alliance juzi usiku Ikulu jijni Dar es salaam.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete ametunukiwa tuzo na Taasisi ya Kimataifa ya Gavi Alliance kutokana na
mchango wake mkubwa kwa jamii wa kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito
na watoto vinavyotokana na tatizo la uzazi vinapungua hapa
nchini.
Tuzo hiyo ilitolewa jana
usiku katika Hoteli ya Serena na Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi hiyo Dagfinn
Hoybraten wakati wa hafla ya utoaji tuzo ilienda sambamba na mkutano wa
kimataifa wa siku tatu wa Gavi Alliance unaoendelea jijini Dar es
Salaam.
Akiongea kabla ya
kukabidhiwa tuzo hiyo Mwanamuzi maarufu wa Afrika ya Kusini Yvonne Chakachaka
ambaye pia ni Balozi wa heshima wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia
watoto Duniani (UNICEF) na mshereheshaji wa shughuli hiyo alisema kuwa hivi sasa
wake wa marais wamekuwa wakijitoa kuisaidia jamii hasa katika mambo yahusuyo
afya ya mama wajawazito na mtoto.
Mke wa rais wa Zambia Dk.
Christine Kaseba Sata naye alipewa tuzo kama aliyopewa Mama
Kikwete.
Aidha Wizara za Afya na
Ustawi wa Jamii pamoja na Fedha zilipewa tuzo kwa ajili ya kuandaa mkutano huo
wa kimataifa wa Umoja wa wadau wa chanjo na Kinga Duniani uliohudhuriwa na
wataalamu wa afya, mawaziri wa afya na wake wa marais kutoka barani
Afrika.
Mama Kikwete kupitia
Taasisi yake ya WAMA amekuwa akitoa vifaa tiba katika Zahanati, vituo vya afya
na Hospitali hapa nchini, kutoa elimu kwa jamii na wataalamu wa afya juu ya
uzazi salama na afya ya mtoto , wanafanya program ya kupunguza maambukizi ya
Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambayo inasaidia mtoto
kuzaliwa salama ingawa wazazi wake wanakuwa na maambikizi.
Pia wamekuwa wakiwawezesha
wanawake kiuchumi katika miradi mbalimbali jambo ambalo limewafanya waweze
kupata kipato cha ziada na hivyo kupunguza makali ya maisha na kuweza kuwatunza
watoto wao kwani wanawake wengi wenye kipato cha kutosha wanaweza kuwatunza
vizuri watoto wao na kupunguza vifo vinavyoepukika.
|
Loading...
Post a Comment