Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya akihutubia wananchi wa kata ya Matanga leo katika ziara yake ya siku 8
kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani Rukwa. Ziara hiyo itahusisha
Wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi pamoja
na
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea maelezo ya shamba darasa
kutoka Afisa Ugani Kata ya Matanga Ndugu Edith Shirima leo alipoanza ziara
yake Mkoani Rukwa kwa kuanzia katika kata hiyo. Kulia ni Afisa kilimo Manispaa
ya Sumbawanga Ndugu George Lupilya, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Sumbawanga.
Kushoto ni Katibu wa Mkuu huyo Mkoa Frank Mateni.
Shamba
darasa katika kata ya Matanga kijiji cha matanga linalomilikiwa na Mkulima mdogo
Bibi Paschalia Ntinda. Mbolea ya kupandia iliyotumika ni Minjingu
Mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akisalimiana
na Bibi Paschalia Ntinda amabaye ni mmiliki wa shamba darasa hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kushoto akisalimiana na wananchi
wakulima katika kata ya kasense leo alipoenda kukagua mashamba darasa katika
kata hiyo. Kata ya Kasense ipo katika Manispaa ya
Sumbawanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akishiri katika palizi ya mahindi
na kinamama wakulima wa kata ya Kasense leo akiwa ziarani katika kata hiyo kwa
ajili ya kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani Rukwa.
Ziara
hii ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa inaenda sambamba na chanjo ya minyoo na vitamin A
kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Kwa kuunganisha zoezi hili na ziara yake
kunatoa fursa kubwa kwa wananchi hususani wa vijijini kuwafikisha watoto wao
kupata chanjo hizo kwa wingi na kirahisi. Katika kata ya Matanga yenye vijiji
vitatu jumla ya watoto 86 walipatiwa chanjo hiyo.
Muuguzi Msaidizi Manispaa ya Sumbawanga Bi Shangwe
Blaya akimpa mtoto Ezeckiel Chokola chanjo ya vitamin A katika kata ya Matanga
ulipofanyika Mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na wananchi wa Kata hiyo
leo.
Halmashauri
zake. Ziara yake inabeba ujumbe huu ufuatao:
1. Mkuu
wa mkoa wa Rukwa anawatakia kila la kheri wananchi wote katika kusherekea
sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya. Anawaomba kudumisha amani, Upendo na Mshikamano
kwenye maeneo yetu na tupashane habari. Toa taarifa Polisi kwa jambo lolote
lisilo la kawaida. Tuwatambue wageni wote wanaofika katika maeneo yetu wengine
si watu wema.
2. Mkuu
wa mkoa anawataka viongozi wote katika ngazi zote kuwajibika na kuwa waadilifu
katika kutimiza wajibu wao.
3. Kila
familia ihakikishe kuwa inatumia fursa hii ya msimu wa mvua katika kujiondoa na
balaa la njaa na pia umaskini wa kipato. Viongozi wa kata na vijiji wafuatilie
ili kujua kila kaya imelima kiasi gani katika msimu huu. Kila kijiji kiwe na
Daftari la wakulima. Wakulima watashindanishwa.
4. Kila
kijiji kitenge maeneo maalum kwa ajili ya kuendeleza shughuli maalum kama
Ufugaji, kilimo na kuchague nguzo yake kuu ya uchumi. (Mpango wa
SAGCOT).
5. Watoto wote watakaofaulumwaka huu wa 2012 lazima
wapelekwe shule. Watoto wa kike wanastahili kulindwa ili wasipate ujauzito.
Mzazi awe mlinzi namba moja.
6. Akina
mama wapeleke watoto wao wa chini ya miaka mitano ili kupata chanjo ya minyoo na
Vitamin A.
7. Kuanzia mwezi wa Januari 2013 watoto wa miezi 9
watapatiwa chanjo ya kuzuia kuharisha na Kichomi. Hivyo wazazi wote tuwapeleke
watoto kupata chanjo hiyo. Malengo yetu ni kuwapa chanjo watoto
wote.
8. Lishe
bora ni muhimu kwa familia. Kula samaki mboga mayai, wanga na nyama kadiri
inavyowezekana.
9. Nawashukuru kwa jinsi mnavyoniunga mkono, nami
nawapenda sana.
Post a Comment