Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo,(WAMA,) akiwapungia mkono watoto yatima (hawapo pichani)
walihudhuria sherehe ya mwisho wa mwaka iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi
hiyo karibu na Ikulu jijini Dar tarehe 8.12.2012.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na
mtoto mlemavu wa ngozi aliyekuwa miongoni mwa watoto yatima walioalikwa kwenye
sherehe ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na taasisi yake kwa kushirikiana
na Kampuni ya Saruji ya Twiga na Dar North Rotary Club kutoka vituo vya Malaika
Orphan Centre (Mkuranga), Mwandaliwa Islamic Orphan Centre (Boko), Umra Orphan
Centre (Magomeni), Kurasini National Orphan Centre na Mama Lenga
(Kigogo).
Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma
Kikwete akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga Bwana
Pascal Lesoinne kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa katika
baadhi ya vituo vya Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi za
WAMA tarehe 8.12.2012.
Baadhi ya watoto yatima wakipata chakula cha
mchana walichoandaliwa na Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na
Mkurugenzi Mkuu wa Twiga Cement Bwana Pascal Lesoinne mara baada ya sherehe ya
mwisho wa mwaka waliyowaandalia watoto yatima kwenye ofisi za WAMA tarehe
8.12.2012.
Post a Comment