Mkurugenzi Mtendaji wa
Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa,
akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu
wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja.
Mafunzo hayo yanahusisha wanaandishi wa habari kutoka nchi zote wanachama wa
EAC, na kufanyika Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa,
akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu
wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja.
Wengine pichani ni washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu wa baraza la
Asasi za Kijamii la Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Martin Mwodha, akizungumza
katika mafunzo hayo juu ya ushiri wa Asasi za kiraia katika ulelimishaji na
ufikishaji wa elimu ya Soko la Pamoja la EAC.
Mchambuzi wa Siasa za
Afrika ambaye pia ni Mwanahabari Mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu
akitoa mada katika mafunzo hayo leo.
Dawati la ufundi nalo
wakati wote lilikuwa katika wakati mgumu wakuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Kutoka kushotoni Aline Ellermann, Elizabeth Wanyoike na Hussein Karim wote
kutoka ofisi ya GIZ ambao ndio wawezeshaji mafunzo hayo yaliyoandaliwa pamoja na
AC
Kuna wakati mambo
yanaonekana hayaendi na hapa anaonekana Elizabeth Wanyoike (kulia) akikuna
kichwa) huku Aline Ellermann akiendelea na kazi.
Fiona Mbabazi kutoka
Rwanda akimshukuru Ofisa mtendaji wa EABC, Andrew Kaggwa kwa maelezo juu ya
Baraza hilo.Kati ni Jenerali Ulimwengu na Aline Ellermann.
Bizimana Jean-Marie
akitoa zawadi kwa Dk. Martin Mwadha wa Asasi za Kiraia za EAC, wengine pichani
kutoka kushoto ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ, Balozi Jeremy Ndayiziga, Andrew
Kaagwa na Jenerali Ulimwengu
Post a Comment