Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Bw Nelson Mandela ametoka Hospitali ambako alikuwa akitibiwa figo na kibofu, msemaji wa serikali amethibitisha, hata hivyo atakuwa akipata matibabu mengine ya kiafya akiwa nyumbani kwake.
Mandela alikuwa
hospitalini tangu Desemba 8 na amekuwa akiripotiwa mara kwa mara kuendelea vema
lakini madaktari wamekuwa wakifanya kazi ya ziada kuhakikisha afya yake inakaa
sawa kutokana pia na umri wake
Baba huyo wa taifa la
Afrika ya kusini ametolewa jana na atakuwa katika uangalizi wa hali ya juu akiwa
nyumbani kwake katika jiji la Johannesburg katika eneo la Houghton mpaka hapo
madaktari watakaporidhika. Msemaji kutoka ofisi ya Rais Mac Maharaj
alisisitiza.
Juzi, Rais Jacob Zuma,
alikuwa ni miongoni mwa watu walioungana na mke wa Mandela, Bi Graca Machel
kumtakia Krismas njema Bwana Mandela katika tafrija fupi iliyofanyika
hospitalini alikokuwa amelazwa katika mji mkuu wa nchi hiyo wa
Pretoria.
Maharaj amechukua wasaa
huu kuwashukuru wananchi na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikitoa
ushirkiano katika kipindi chote cha matatizo ya kiafya ya bwana
Mandela
Post a Comment