Mbunge wa Arusha Mjini-CHADEMA,Godbless Lema akisalimia
wananchi wa Arusha jana
---
Na Mroki Mroki-Arusha
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema
amewaahidi wapiga kura wake kutoendelea na siasa za maandamano na badala yake
sasa ni kazi tu na mijada la malalamiko yote ni katika
vikao.
Akihutubia wananchi, alisema yuko tayari kuwatumikia
Wana-Arusha huku akiahidi kuwa hatoandamana tena, bali madai na kero zake
atazielekeza kwenye vikao ndani ya Halmashauri.
Alisema akiwa madarakani, hatapenda kuona watu
wakiteswa na wanamgambo wa Jiji, hasa wanawake na wafanyabiashara ndogoo na
kusisitiza kuwa, hayasemi hayo kwa lengo la uchochezi, bali kama angalizo kwa
kuwa siku zote yupo kwa ajili ya kupigania haki na hatarudi nyuma kwa hila
yoyote.
Kabla ya kukaribishwa kuzungumza na wananchi, Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema chama chake kimefanya tathimini ya kesi iliyomalizika na kusema wanatarajia kudai fidia ya gharama za kesi hiyo inayofikia Sh milioni 253.
Golugwa pia alitumia muda huo kumkabidhi bendera ya Bunge Lema ambayo alikabidhiwa na Mbunge huyo baada ya kuvuliwa nafasi hiyo Aprili mwaka huu.
Alisema alipokabidhiwa bendera hiyo alimwambia aiweke na kusubiri Mungu atende muujiza ambao kwa sasa anasema umetimia kwa Lema kurudishiwa ubunge.
Kuhusu madiwani waliofukuzwa Chadema, alisema kuwa bado anaamini walitendewa haki ya kufukuzwa sababu ya kurubuniwa na huku akiahidi kuwa, uchaguzi ukirudiwa chama chake kitaibuka na ushindi mnono.

Post a Comment