Na
Waaandishi wetu , hudumabongo@gmail.com
Uchunguzi
uliofanywa na wanahabari katika zoezi la kukusanya kero za sekta binafsi
linaondelea kupitia mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook umeonyesha kuwa
wakazi wa jijini Dar es Salaam wanakabiliwa na mgao wa umeme kwa kipindi kirefu
sasa.
Hali hiyo
imebainika wakati wa majumuisho ya kero za wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali
nchini Tanzania katika mzunguko wa tatu ambapo Shirika la Ugavi wa
Umeme TANESCO limechukua nafasi ya kwanza kati ya biashara 36 zilizotajwa kuwa
kero kwa wateja.
Jumla ya
kero tofauti 220 zimewasilishwa na wateja toka zoezi hilo lianze ambapo Shirika
la Tanesco lina jumla ya kero 71 ambapo kati ya hizo 60 ni kutoka Dar es Salaam
pekee. Katika mzunguko huu nafasi ya pili ilishikiliwa na Kampuni
ya Mawasiliano ya Tigo yenye kero 63 kati ya 220 huku nafasi ya
tatu ikiwaendea Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom yenye kura 17
kati ya 220 zilizowasilishwa.
Hakukuwa
na mabadiliko makubwa katika makundi mengine ambapo washindi wa kero ni wafuatao
Precision Air ( Huduma za Anga) CRDB ( Huduma za Kibenki)
StarTimes (Ving’amuzi) DAWASCO ( Huduma za Maji Safi na Taka mkoani DSM)
SHOPRITE- ( Wauzaji wa bidhaa
mbalimbali)
Katika
mzunguko huu jumla ya biashara 4 zimeingia katika mchuano huo nazo ni Mara Milk,
Zanzibar Insurance, Bonjour Petrol Station na Coca Cola (Nyanza
Bottlers)
Kwa
maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea
link ifuatayo http://bit.ly/10SARH1
Huduma
Bongo inatoa wito kwa vyombo vya habari nchini kufuatilia kwa makini kero hii ya
mgao wa umeme unaofanyika kwa siri na utaalamu wa hali ya juu na kuleta usumbufu
mkubwa kwa wanajamii na hasara kwa wafanyabiashara.
Post a Comment