 |
Katibu wa
Azam, Nassor Idrisa (kulia) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, kiungo wao mpya,
Humphrey Mieno waliyemsajili kutoka Sofapaka ya Kenya. Mieno ameungana na kikosi
cha Azam mjini hapa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako timu
hiyo imekuja kucheza Kombe la Hisani. Mieno alikuwepo kwenye kikosi cha Kenya,
Harambee Stars kilichofika fainali ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge wiki
iliyopita na kufungwa 2-1 na wenyeji Uganda, The Cranes. Amepewa jezi namba 30,
ambayo iliwahi kuvaliwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ aliyehamia SImba
SC.
|
chanzo: Bin Zubeiry
on Saturday, December 15, 2012
Post a Comment