TAARIFA KWA
WANAYANGA.
Klabu ya
Young Africans ilikuwa ifanye mkutano Wanachama tarehe 08 Disemba 2013, kama
ilivyokua imetangazwa na Uongozi hapo awali. Tunapenda kutoa taarifa kuwa tarehe
ya mkutano huo sasa imebadilishwa na kusogezwa mbele hadi tarehe 19 Januari 2013
kwa sababu zifuatazo:
1.Kutoa
nafasi kwa Wanachama na Wapenzi wa YANGA kushirki kikamilifu maandalizi ya
sherehe za Uhuru wa Taifa letu zitakazofanyika tarehe 09, Disemba 2012,
na
2.Tuko
katika mazungumzo na Kampuni moja maarufu ya kusimamia shughuli za mkutano huo
kwa upande wa ufadhili, ili kuweza kutunisha mfuko na Klabu kujiingizia mapato
kati ya shilingi za Kitanzania 200,000,000/= (shilingi milioni mia mbili tu)
hadi 350,000,000/= (shilingi milioni mia tatu hamsini tu) na Kampuni husika
wameomba kuongezewa muda ili waweze kufanya hiyo kwa ufanisi
mkubwa.
Tunapenda
kuwashukru Wanachama na Wapenzi wa YANGA kwa mshikamano na umoja uliopo. Tuzidi
kuijenga Yanga kwa maendeleo na mafanikio daima.
"YANGA
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO"
YUSUF
MEHBUB MANJI
MWENYEKITI
YOUNG
AFRICANS SPORTS CLUB
Post a Comment