Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MOTO
umeendelea kuwaka kati ya mmiliki wa Kampuni ya Mc Donald Live Line Technology
Ltd, Mc Donald Mwakamele kwa kumtaka Mbunge wa Ubungo, kwa tiketi ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, aache kumkimbia badala yake
athibitishe hoja anazotoa.
Mc
Donald Mwakamele
Kwa
wiki kadhaa sasa, wawili hao wamekuwa wakirushiana makombora, baada ya Mnyika
kusema kuwa Mwakamele ni fisadi aliyepewa tenda nyingi katika Shirika la Umeme
la TANESCO, likiwa chini ya William Mhando.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Mwakamele alisema anamshangaa Mnyika kuendelea kupiga kelele ili
ajijenge kisiasa, huku akishindwa kuweka ushahidi mezani.
"Mnyika
aache kunikimbia na kama kweli ana hoja za msingi basi atangaze, maana
nilishamwambia kuwa akithibitisha ukweli wake huo, atampa Milioni 20, ingawa
ameshindwa na kubaki kupiga kelele,” alisema.
Mkurugenzi huyo wa Mc Donald
aliyefanya kazi katika Shirika la Umeme kwa zaidi ya miaka 20, alisema badala ya
kuendelea kupiga porojo kumnufaisha kisiasa, akutane naye, kuzungumzia hilo ili
ukweli ujulikane na iwe nafasi kwa mbunge huyo kuwatumikia vyema wananchi wa
Ubungo waliyomuweka madarakani.
Alisema
Mnyika hana uwezo wowote wa kupambanua mambo zaidi ya kupiga soga na kuwaweka
kwenye wakati mgumu wananchi wake wanaoishi maisha magumu, huku mbunge wao
akibwabwaja mitaani, ndio maana ameshindwa kujenga hata choo kwa ajili ya
wananchi wake Ubungo, huku akipenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari akiamini
ni mtaji wake kisiasa.
“Inashangaza, maana huu ufisadi
unaozungumzwa na Mnyika ulifanyiwa uchunguzi na serikali. Sasa labda Mnyika
aseme anataka mimi mtuhumiwa nijitangaze mwenyewe wakati anajua fika mambo haya
yana wazungumzaji wao.
“Harakati za Mnyika zinashangaza,
hivyo labda aniambie kuwa madai yake nimwambie yeye kwa serikali gani aliyokuwa
nayo? Ipo serikali yenye viongozi makini, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo, anayefanya fanya kazi kwa ajili ya Watanzania wote,
hivyo Mnyika aache siasa uchwara kwa kupiga porojo akiamini kuwa Watanzania
wanapenda maneno yake,” alisema.
Mwakamele alisema kutwa na refarii
kwenye kazi zozote ni jambo la msingi, hivyo yeye haoni sababu kuwa na refa
Mhando, hasa kwenye kazi za Kimataifa.
“Sio
kila wakati tunakiwa tufanye siasa, maana haya madai ya Mnyika yameshawahi
kutokea Tanesco kwa kusimamisha uchukuaji wa nguzo katika kampuni za Kitanzania,
ikiwamo ya Saohill ya Mafinga hadi Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene kupiga marufu suala hili.
“Mbali
na hilo, kama utakumbuka Tanesco pia iliingia kwenye utata wa Richmond kwa
kusimamisha mradi wao ambao baadaye ukawa mzigo mkubwa kwa serikali, hivyo
wanasiasa wanapovaa vibwaya katika suala la ufisadi wawe na uthibitisho badala
ya kuzungumza kwa kujua vyombo vya habari vitanukuu,” alisema.
Alisema
katika kuhakikisha kuwa Taifa linapiga hatua, ameweza kufungua Chuo cha Umeme
bila kuzima, akiamini kuwa mabilioni ya shilingi yataokolewa endapo teknolojia
hiyo itatumiwa na Tanzania nzima, ingawa mgogoro mkubwa umeibuka kutokana na
baadhi ya mabosi wa Tanesco kuipiga vita na Tanesco mkoani Morogoro kuuzima
umeme katika njia inayokwenda kwenye chuo chake, alipotembelewa na wageni kutoka
nchi mbalimbali duniani waliokwenda kushuhudia teknolojia hiyo inayoendeshwa na
Mtanzania.
Mwakamele alisema anashangaa
mbunge huyo kwa kuwa mwepesi kwenye vyombo vya habari, wakati alimtaka waonane
uso kwa uso na kukataa, hata pale alipotangaza ofa ya milioni 20 ili atangaze
ufisadi huo.
chanzo: Handeni Kwetu
Post a Comment