Mbunge wa Jimbo la Ubungo
(Chadema), John Mnyika.
ORODHA YA AWAMU YA KWANZA: JUU YA MASUALA NA MATUKIO YA UFISADI NA UZEMBE YALIYOHUSU MIKATABA YA MAKAMPUNI YA M/S SANTA CLARA SUPPLIES COMPANY LIMITED NA M/S McDONALD LIVE LINE TECHNOLOGY LIMITED.
Masuala na matukio ya ufisadi na uzembe yaliyohusu mikataba ya
makampuni ya M/s Santa Clara Supplies Company Ltd na M/s McDonald Live Line
Technology Limited ambayo yamefanyika kinyume na sheria
mbalimbali.
Kwa ushahidi wa nyaraka baadhi ya sheria zilizokiukwa ni pamoja na
Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2004, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya
mwaka 2004, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na sheria
nyinginezo. Aidha, masuala na matukio ya ufisadi na uzembe katika mikataba hiyo
yamefanyika kinyume na kanuni, miongozo na maadili ya Shirika la Umeme
(TANESCO).
Ufisadi na uzembe umesababishwa na makosa mengine mbalimbali
mathalani mgongano wa kimaslahi, utovu wa uaminifu, matumizi mabaya ya ofisi na
makosa mengine yaliyo kinyume cha sheria na maadili ya viongozi na watumishi wa
umma.
Orodha ya wanaotuhumiwa kuhusika katika ufisadi na/ama uzembe huo 18
ni kama ifuatavyo:
<!--[if !supportLists]-->1.
<!--[endif]-->Mhandisi WILLIAM GEOFREY MHANDO
Huyu alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme Tanzania
(TANESCO) na ndiye mtuhumiwa mkuu wa ufisadi unaohusu mikataba tajwa.
Akiwa mkurugenzi mkuu wa TANESCO aliingia mkataba na kampuni ya SANTA
CLARA kwa tenda No PA/001/11/HQ/G/011 kuleta vifaa vya ofisini, kwa kipindi
hicho kampuni hiyo tajwa hapo juu ilikuwa inamilikiwa na wanahisa ambao ni
familia ya Mhando mwenyewe.
Mkataba huo ulisainiwa na mkewe kama mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo
ya CLARA, kitendo hicho cha mkurugenzi kuipatia kampuni ya mkewe tenda ni
kinyume na maadili ya Tanesco kifungu cha 2.2, ni kinyume na Sheria ya Ununuzi
ya umma kifungu cha 33, 73(3) na 73 (5) pamoja na sheria ya maadili ya viongozi
wa umma kifungu cha 6 (d), (e) kutokana na kuwa na mgongano wa maslahi na utovu
wa uaminifu.
Aidha kusaini kwa mkataba huo yeye akiwa mkurugenzi wa TANESCO ni
matumizi mabaya ya ofisi, kwa kutumia ofisi ya umma kujinufaisha yeye pamoja na
familia yake na kushindwa kusimamia sheria zinazoongoza na kusimamia ununuzi wa
umma.
Kwa upande mwingine, aliingia katika makubaliano na Donald George
Mwakamele (mkurugenzi na mwanahisa katika kampuni ya McDONALD) makubaliano
ambayo hayaruhusiwi na yenye mgogoro ( Conflicting Joint Venture Agrement)
kinyume na maadili ya TANESCO na sheria nyingine za nchi nilizozitaja
awali.
Lakini pia akijifanya ni mfanya biashara alisaini na makubaliano na
kampuni hiyo makubaliano ya pande mbili ya kutafuta tenda, kununua, kujenga,
kufanya matengenezo na kufanya miradi yote inayohusika na umeme. Katika
kuwezesha hilo Mhando alikuwa na jukumu la kutafuta miradi ya umeme na endapo
ikikamilika pande hizi mbili zinagawana mapato na faida inayotokana na miradi
hiyo wakati huo huo yeye akiwa mtumishi wa TANESCO.
Pamoja na kufukuzwa kazi, umma unapaswa kuunganisha nguvu kutaka
Mhando achunguzwe kwa makosa ya kijinai kutokana na tuhuma za ufisadi
zinazomhusu na kufunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria za
nchi.
<!--[if !supportLists]-->2.
<!--[endif]-->Bw. HARUN MATTAMBO
Huyu ni Afisa ugavi wa shirika la umeme Tanzania ( TANESCO) amefanya
uzembe kwa kushindwa kuhakikisha manunuzi yote yanayofanywa na shirika
yanazingatia taratibu na kutimiza sheria za manunuzi ya
umma.
Aliruhusu kufanyika kwa ufisadi na ukiukwaji wa sheria katika
kupatikana kwa zabuni na. PA/001/11/HQ/G/011 na kuathiri Shirika la Umeme
(TANESCO).
Alipendekeza kampuni ya M/s Mc Donald ipewe mkataba pamoja na kuwa
haikuwa imetimiza masharti ikiwemo kukwepa kuwasilisha mahesabu ya fedha
yaliyokaguliwa ya mwaka 2009 kama sheria ilivyohitaji.
Matokeo ya uzembe wake wa kuruhusu ufisadi ni kulisababishia hasara
Shirika la Umeme (TANESCO) kwa kuwa kampuni hiyo ya Mc Donald ilipatikana bila
kushindanishwa na makampuni mengine yaliyokuwa na unafuu na yaliyotimiza
masharti.
Umma uungane kutaka Matambo afukuzwe kazi mara moja, na kuchunguzwa
kuhusu tuhuma za kufanya uzembe huo kwa lengo la kujinufaisha na kunufaisha
washirika wake kwa ajili ya hatua za ziada za kisheria.
<!--[if !supportLists]-->3.
<!--[endif]--> Bw ROBERT SHEMHILU
Huyu aliwahi kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa TANESCO na anatuhumiwa
kufanya uzembe ulioruhusu ufisadi.
Alifanya makosa ya kuruhusu malipo yaliyofanyika tarehe 5 Septemba
2011 kabla hata ya kusainiwa kwa mkataba na kuruhusu kuletwa kwa vifaa kabla
hata ya kusainiwa kwa mkataba katika ya TANESCO na kampuni iliyopewa kinyemela
zabuni ya kuleta vifaa.
Alifanya pia makosa ya kuilipa kampuni ya Mc Donald malipo ya juu ya
asilimia 30 ya thamani ya mkataba wakati vifungu vya 26 na 54.1 vya mkataba huo
(pamoja na kuingiwa kinyemela) vilielekeza malipo ya asilimia 15
tu.
Shemhilu pamoja na kusimamishwa umma uunganishe nguvu kutaka,
afukuzwe kazi mara moja na kuchunguzwa kwa ajili ya hatua za
ziada.
<!--[if !supportLists]-->4.
<!--[endif]-->FRANCE MCHALANGE, NAFTARI KISIGA NA SOPHIA
MSIDAI
Hawa walifanya uzembe wa kushindwa kusimamia Sheria ya Ununuzi wa
Umma pamoja na maadili kwa kupendekeza kwamba Kampuni ya SANTA CLARA ipewe
zabuni ya kuuzia vifaa TANESCO pamoja na kufahamu kuwa kampuni tajwa ilikuwa
haijatimiza masharti na kulikuwa na mgongano wa maslahi.
Umma uhakikishe wanachukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na kukiuka
sheria ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa umma kuwajibika kutoa
mapendekezo kwa kuzingatia sheria na maslahi ya umma.
<!--[if !supportLists]-->5.
<!--[endif]-->Mhandisi DECLAIN MHAIKI na Bw SUKE
Akiwa mtumishi wa umma alizembea na kukwepa kutoa taarifa kuhusu
kukiukwa kwa vigezo na masharti kuhusu zabuni na. PA/001/09/HQ/W/014 na kufanya
kampuni ya McDonald Live Line Technology ipatiwe zabuni kinyume cha sheria ya
ununuzi wa umma ya mwaka 2004.
Aidha alichangia kufanya kampuni hiyo kupewa zabuni pamoja na kuwa
haikuwa na uwezo wa kifedha na kuiwezesha kupewa malipo ya asilimia ya ziada
kinyume na mkataba. Huyu naye umma uhakikishe wanachukuliwa hatua za kinidhamu
kutokana na kukiuka sheria na mkataba.
<!--[if !supportLists]-->6.
<!--[endif]-->Mhandisi D. MHAIKI, S.NKONDOLA, N.NTIMBA.Mhandisi CHEGERE, MAKIA NA
MWITA.
Wote kama timu walifanya maamuzi yaliyosababisha kutolewa kwa mkataba
na. PA/001/HQ/W/14 wa tarehe 11 Machi 2010 kwa kampuni ya Ms. Donald Live Line
Technology bila kuzingatia uwezo wa kitaalamu, kifedha na masharti mengine na
hivyo kukiuka sheria ya ununuzi ya umma na kushindwa kulinda maslahi ya
taifa.
Hawa wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinadhamu ili kudhibiti maamuzi
na mapendekezo ya wataalamu katika utumishi wa umma kuingiza mashirika ya umma
na nchi katika mikataba mibovu ili kupanua wigo wa
uwajibikaji.
<!--[if !supportLists]-->7.
<!--[endif]-->FATUMA CHUNGU, ATHANASIUS NANGALI, ELANGWA
MGENI
Kundi hili limehusika katika majadiliano na kutoa mapendekezo
yaliyowezesha kampuni ya McDonald kupewa mkataba
kinyemela.
Iwapo kundi hili lisingefanya uzembe na kusababisha ukiukwaji wa
sheria mchakato wa mkataba huo kati ya mwezi Machi mpaka Mei 2009 ungewezesha
TANESCO kuingia mkataba na kampuni yenye uwezo na iliyotimiza masharti na
kuepusha shirika hilo kupata hasara na kubeba gharama ambazo zingeweza
kuepukika.
Ni muhimu wakachukuliwa hatua za kinadhamu ikiwa ni sehemu ya
kuchangia katika kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa umakini na
ueledi ili kuepusha TANESCO kuendelea kufanya majadiliano na kuingia mikataba
mingine mibovu yenye kuongeza mzigo wa gharama kwa shirika na hatimaye ongezo la
bei kwa wananchi.
<!--[if !supportLists]-->8.
<!--[endif]-->LUSEKELO KASSANGA (MKURUGENZI WA FEDHA)
Huyu alibariki ufisadi wa malipo yenye mkanganyiko katika TANESCO kwa
kuilipa kampuni ya Santa Clara mapema kabla hata haijafanyiwa tathmini na
kupatiwa zabuni.
Malipo yalifanyika kinyemela tarehe 5 Septemba 2011 wakati ambapo
tathmini ya zabuni ilifanyika tarehe 23 Septemba 2011, maana yake ni kwamba
malipo yalifanywa kabla hata kampuni husika haijapewa kazi kwa mleta vifaa asiye
na uwezo na mwenye mgongano wa kimaslahi.
Kassanga anapaswa kufukuzwa kazi na kuchunguzwa kuhusu tuhuma za
ziada za kunufaika kutokana na baadhi ya malipo yaliyofanywa kwa makampuni
mbalimbali wakati akiwa mkurugenzi wa fedha ili aweze kuchukuliwa hatua zaidi za
kisheria.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika
Mbunge wa Jimbo la Ubungo
09/12/2012
Chanzo: Mnyika Blog
Post a Comment