Mazungumzo baina ya ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pamoja na waasi wa kundi la M23 yameanza yanaendelea mjini Kampala Uganda, chini ya usuluhishi wa mwenyekiti wa nchi za kanda ya maziwa makuu.
Mazungumzo hayo yameendelea, licha ya mkasa uliotokea juzi, baada ya ujumbe wa waasi kuilaumu serikali ya Kongo kuwa inawafadhili waasi kutoka nchi jirani na walio tishio kwa usalama wa nchi hizo pamoja na raia wa mashariki mwa Kongo.