Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Viongozi Uamsho Waanza Kutendewa Haki Mahabusu


 

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kushoto ni Azzan Khalid Hamdan, Msellem Ali Msellem, Farid Hadi Ahmed, Khamis, na Mussa Juma Issa wakiwa katika Msikiti wa Mbuyuni
UONGOZI wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar (Magereza) umeanza kuwapatia huduma muhimu Viongozi wa Uamsho kama wanavyopatiwa mahabusu wengine wakiwa mahabusu katika gereza la kinua miguu mjini Zanzibar, imefahamika jana …

Hayo yameelezwa na Wakili wa washitakiwa hao Salum Toufiq, kabla ya kuanza kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na Viongozi hao ya kupinga kubaguliwa kupewa huduma bora tangu kufunguliwa mashitaka na kusababisha uharibifu wa mali na kuhatarisha usalama wa Taifa Oktoba 21 mwaka huu.
Alisema kwamba wateja wake tayari wameruhusiwa kula chakula kutoka nyumbani, kusoma misahafu, kubadilisha nguo, pamoja na kuchaganyikana wao kwa wao badala ya kufungiwa kila mshitakiwa na chumba chake(selo).
Hata hivyo alisema kwamba wateja wake bado hawajapata haki ya kukutana na jamaa zao wakiwemo wake zao, lakini alisema kwamba inawezekana pia wakapatiwa haki hiyo.
Katika hatua nyingine upande wa mashitaka jana umewalirisha pingamizi wakitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar, kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa na viongozi nane wa Uamsho ambao wanapinga dhamana yao kufungwa na Mkurugenzi wa mashitaka Zanzibar (DPP) pamoja na kunyimwa huduma bora wakiwa mahabusu.
Mwendesha mashitaka wa serikali Ramadhan Nasib, alidai kwamba kesi hiyo imefunguliwa kinyume na sheria kutokana na hati ya kiapo kukosa tarehe ya kufunguliwa pamoja na jina la mtu aliyekula kiapo kwa niaba ya washitakiwa hao.
Aidha alidai kwamba upande wa utetezi katika kesi hiyo umeshindwa kueleza katika hati ya kiapo wametumia kifungu gani cha sheria katika kufugua kesi hiyo.
“Katika hati ya dharura kuna nyaraka zimewasilishwa Mahakamani zina makosa ambayo hayarekebishiki kisheria kwa sababu hati ya dharura haina mawasiliano (Correspondent) kama taratibu za sheria zinavyosema” Alisema Nasib, akisaidiwa na mwanasheria Raya Mselem Issa.
Aidha alisema kwamba upande wa utetezi hawakupaswa kufungua ombi la kutaka Mahakama Kuu kufanya mapitio juu ya uamuzi uliyotolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu na kusikilizwa na Jaji mwengine badala ya mrajisi ambaye ndiye alitoa maamuzi hayo kwa mujibu wa sheria.
“Kesi ya msingi haipo mbele yako Jaji, kesi ipo kwa Mrajisi wa Mahakama Kuu tena ipo katika hatua ya kwanza ya kutajwa na mapitio ya uamuzi yalitakiwa kufanywa na Mrajisi mwenyewe sio maahakama yako,”alisema Mwansheria Raya Mselem Issa kutoka Ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka Zanzibar.
Hata hivyo jopo la mawakili wakiongozwa Salum Toufiq, Rajab Abdallah, Abdalla Juma Mohamed na Suleiman Salum, walipinga madai hayo na kutetea hoja yao kuwa hati ya kiapo imetayarishwa kwa kuzingatia taratibu za kisheria licha ya nyaraka nyingine kukosekana tarehe na jina la mtu aliyekula kiapo kwa niaba ya Viongozi wa Uamsho.
Wakili Rajab alisema kwamba kama kuna kasoro sio sababu ya msingi kwa wateja wake kutosikilizwa kesi ya msingi hasa kwa kuzingatia haki za wateja wao zimekuwa zikivunjwa tangu kufunguliwa mashitaka.
“Mheshimiwa huwezi kuaihirisha kufunga ndoa kwa sababu tu ya bwana harusi hajavaa kiremba, sio vizuri wenzetu kuwaita waongo lakini hawasemi ukweli juu ya hati ya kiapo” alisema wakili Rajab.
Alisema kwamba kama kuna kasoro katika hati ya kiapo Mahakama inaweza kuweka kando maeneo yenye kasoro na kusikiliza hoja ya msingi ya wateja wake ya kufungua kesi hiyo.
Pingamizi hilo la upande wa mashitaka limesikilizwa kwa muda wa saa nne na Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Mkusa Isack Sepetu ambaye amepanga kutoa hukumu yake Desemba 19 mwaka huu.
Viongozi waliofungua kesi hiyo ni Sheikhe Farid Hadi Ahmed(41), Mselem Ali Mselem(52), Mussa Juma Issa(37), Azzan Khalid Hamdan(48), Seleiman Juma Suleiman(66), Khamis Ali Suleiman(59), Hassan Bakari Suleiman(39) na Gharib Ahmada Omar(39) ambao ni wakaazi wa Zanzibar.
Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top