Tuzo ya amani ya Nobel imetangazwa jana mjini Oslo, na tunuku hiyo kwenda kwa Umoja wa Ulaya, ukitambuliwa na kamati ya tuzo hiyo, ambayo imetambua mchango wake wa kuendeleza utulivu na demokrasia.
Umoja huo umewatuma marais wake watatu katika sherehe hiyo ya mjini Oslo kupokea tuzo hiyo ya mwaka 2012, ambayo wakosoaji akiwemo mshindi wa zamani Desmond Tutu wanasema haukustahili. Lakini mwenyekiti wa kamati wa kamati ya Nobel, Thorbjorn Jagland amesema kamati yake haikukosea kuupa Umoja huo tuzo hiyo.
Post a Comment