MHANGA wa ubakaji na
mauaji yaliyozusha maombolezo makali pamoja na hasira nchini India amefanyiwa
taratibu za mazishi kwa kaida za Kihindi, kwa kuchomwa tukio lililofanyika kwa
faragha leo Jumapili.
Tukio hilo lilifanyika
saa kadhaa baada ya mwili wa marehemu kurejeshwa nchini humo kutoka
Singapore.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake mwenye umri wa miaka
23, ambaye alisababisha maandamano makubwa nchi nzima tangu aliposhambuliwa
kinyama katika basi mjini New Delhi wiki mbili zilizopita, alichomwa moto bila
kuwapo watu ambao wangeshuhudia tukio hilo kwa ombi la wazazi wake waliokuwa na
fadhaa kubwa.
Mwili wa marehemu
ukichukuliwa katika jeneza.
Taratibu za
mazishi.
Taratibu hizo za mazishi za kuchoma moto , zilifanyika baada ya
ndugu na marafiki kufanya taratibu za mwisho za maombi kwa muda mfupi katika
wilaya ya kusini magharibi ya Dwarka mjini Delhi, kwa mujibu wa waombolezaji
ambao wamemweleza msichana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa taaluma ya udaktari
kuwa alikuwa mtu anayetambulika na wengi na mwenye kipaji.
"Nimekuja kwa
sababu nilikuwa nampenda kwa dhati msichana huyu.
Alikuwa mtu mwenye
uwezo mkubwa kuliko wasichana wengine wote katika eneo tunakoishi," amesema
Meena Rai, ambaye alikuwa rafiki wa karibu na jirani.
Waziri mkuu awataka
Wahindi kuwa watulivu
Waziri mkuu Manmohan Singh na Sonia Gandhi, kiongozi wa
chama kikuu tawala cha Congress, walikuwa katika uwanja wa ndege mjini New Delhi
kuwapa pole wazazi wa msichana huyo wakati mwili wake ulipokuwa ukiwasili
nyumbani kwa ndege ya kukodi ikiwa na mwili wa mtoto wao.
Balozi wa India nchini
Singapore T.C.A Raghavan katika hospitali ya Mount Elizabeth.
Baada ya matibabu ya
awali katika hospitali mjini Delhi , alipelekwa nchini Singapore siku ya
Jumatano usiku.
Lakini madaktari wameshindwa kuzuwia viungo vyake kadha
vilivyoshindwa kufanyakazi na alitangazwa kuwa amefariki katika saa za alfajiri
siku ya Jumamosi Dec29/ 2012.
Kifo chake kilisababisha serikali kuahidi
ulinzi bora zaidi kwa wanawake, na tathmini ya kina kwa taifa hilo ambapo
matukio ya ubakaji hutokea kila siku na udhalilishaji huo wa kingono hupuuziwa
kila mara, kama mchezo wa mzaha tu.
Msichana akishiriki
katika maandamano India
Wimbi la maandamano
lilizuka nchini India tangu shambulio hilo usiku wa Desemba16 wakati mwanamke
huyo alipofanyiwa unyama huo pamoja na kushambuliwa kwa kupigwa kwa chuma, na
kusababisha kupata majeraha mabaya tumboni.
Mishumaa yawashwa kumuenzi
marehemu
Maelfu ya watu walishiriki katika tukio la kuwasha mishumaa usiku
siku ya jumamosi baada ya waziri mkuu Singh kuongoza miito ya kuwataka watu kuwa
watulivu na kuepusha kurejewa kwa maandamano yaliyokuwa na ghasia.
Wanafunzi na
wanaharakati wakishiriki maandamano nchini India
Msichana huyo alitarajia
kuolewa na mpenzi wake ambaye nae alijeruhiwa katika shambulio hilo, amesema
hayo Meena Rai , ambaye amekuwa akifanya ununuzi kwa ajili ya maandalizi ya
haurusi hiyo na marehemu.
Harusi ilikuwa inatarajiwa kufanyika mwezi
Februari mwaka ujao.
MHANGA wa ubakaji na
mauaji yaliyozusha maombolezo makali pamoja na hasira nchini India amefanyiwa
taratibu za mazishi kwa kaida za Kihindi, kwa kuchomwa tukio lililofanyika kwa
faragha leo Jumapili.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake mwenye umri wa miaka 23, ambaye alisababisha maandamano makubwa nchi nzima tangu aliposhambuliwa kinyama katika basi mjini New Delhi wiki mbili zilizopita, alichomwa moto bila kuwapo watu ambao wangeshuhudia tukio hilo kwa ombi la wazazi wake waliokuwa na fadhaa kubwa.
Mwili wa marehemu
ukichukuliwa katika jeneza.
Taratibu hizo za mazishi za kuchoma moto , zilifanyika baada ya ndugu na marafiki kufanya taratibu za mwisho za maombi kwa muda mfupi katika wilaya ya kusini magharibi ya Dwarka mjini Delhi, kwa mujibu wa waombolezaji ambao wamemweleza msichana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa taaluma ya udaktari kuwa alikuwa mtu anayetambulika na wengi na mwenye kipaji.
"Nimekuja kwa sababu nilikuwa nampenda kwa dhati msichana huyu.
Alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko wasichana wengine wote katika eneo tunakoishi," amesema Meena Rai, ambaye alikuwa rafiki wa karibu na jirani.
Waziri mkuu awataka Wahindi kuwa watulivu
Waziri mkuu Manmohan Singh na Sonia Gandhi, kiongozi wa chama kikuu tawala cha Congress, walikuwa katika uwanja wa ndege mjini New Delhi kuwapa pole wazazi wa msichana huyo wakati mwili wake ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwa ndege ya kukodi ikiwa na mwili wa mtoto wao.
Balozi wa India nchini
Singapore T.C.A Raghavan katika hospitali ya Mount Elizabeth.
Lakini madaktari wameshindwa kuzuwia viungo vyake kadha vilivyoshindwa kufanyakazi na alitangazwa kuwa amefariki katika saa za alfajiri siku ya Jumamosi Dec29/ 2012.
Kifo chake kilisababisha serikali kuahidi ulinzi bora zaidi kwa wanawake, na tathmini ya kina kwa taifa hilo ambapo matukio ya ubakaji hutokea kila siku na udhalilishaji huo wa kingono hupuuziwa kila mara, kama mchezo wa mzaha tu.
Msichana akishiriki
katika maandamano India
Wimbi la maandamano
lilizuka nchini India tangu shambulio hilo usiku wa Desemba16 wakati mwanamke
huyo alipofanyiwa unyama huo pamoja na kushambuliwa kwa kupigwa kwa chuma, na
kusababisha kupata majeraha mabaya tumboni.Mishumaa yawashwa kumuenzi marehemu
Maelfu ya watu walishiriki katika tukio la kuwasha mishumaa usiku siku ya jumamosi baada ya waziri mkuu Singh kuongoza miito ya kuwataka watu kuwa watulivu na kuepusha kurejewa kwa maandamano yaliyokuwa na ghasia.
Wanafunzi na
wanaharakati wakishiriki maandamano nchini India
Msichana huyo alitarajia
kuolewa na mpenzi wake ambaye nae alijeruhiwa katika shambulio hilo, amesema
hayo Meena Rai , ambaye amekuwa akifanya ununuzi kwa ajili ya maandalizi ya
haurusi hiyo na marehemu.Harusi ilikuwa inatarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka ujao.
Post a Comment