Kuna baadhi ya wanawake huwa hawawezi kuwaambia waume zao kwamba wanawahitaji kimapenzi, badala yake huweza kujitegesha au kujirahisi mbele zao, kwani wanajua kuwafanyia hivyo kutaamsha hamu kwa waume zao na hatimaye kuipata starehe hiyo pamoja. Mume yakupasa uwe unausoma mchezo mapema kwani si wanawake wote wataweza sema au kujitegesha na ndio maana tunasisitiza isipite wiki bila kupeana na mwenza wako.
Pia wanawake nawashauri wawe
"wachokozi" kidogo maana kuna
wanaume huwa hawaanzi mashambulizi mpaka washambuliwe, kama hali ipo hivyo basi
mwanamke inabidi ndo uwe mpangaji mashambulizi ya awali.Mwisho niwaambie Mke na Mume, kama inavyowapasa kujua sehemu za mihemuko baina yenu, inawapasa pia muelewe lugha za miili yenu. Miili inaongea bwanaa, ipeni nafasi!!!


Post a Comment