Shughuli kubwa iliyofanywa na mtoto mdogo
Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa ngoma ndiyo iliyowafanya baadhi ya viongozi
wa kisiasa na Serikali kuenda kumtunza mtoto huyo, ambapo Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba
walienda na kumtunza mtoto huyo kwa umahiri wake katika kupiga
ngoma.
Jana nilipita maeneo ya Manzese katika moja
ya kiota cha siku nyingi Frieds Coner na kumkuta mmoja wa wanakikundi akiwa na
watoto hao nje ya hoteli hiyo, akajitambulisha kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na
ni msaidizi wa Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye
amefuatana na kikundi hicho kama mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani
Mara.
Kilichinisikitisha sana ni kiongozi huyo
kuonekana akiwa ameshika chupa ya pombe kali aina ya Value akionekana
kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko cha chupa hiyo, huku mtoto
Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa pombe hiyo ikiwa ni kuashiria
kwamba hawezi kumudu kuinywa.
Kitu kilichiniumiza sana nilipoongea na
Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa wazazi wa watoto hao wamebaki Musoma. Hivyo
watoto hao wako chini ya uangalizi wa kikundi hicho pekee jambo ambalo si jema
na kuna uwezekano mkubwa wa kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana
ulinzi wa kotosha kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa pombe hiyo ya
Value na kiongozi huyo.
(NA KIKOSI KAZI CHA
FULLSHANGWEBLOG.COM)


Post a Comment