LONDON, England
Nani, 26, kwa sasa yuko nje ya kikosi kutokana na
matatizo ya nyama za paja, akiwa na salio la mkataba wa miezi 18, ambao
unamuwezesha kupokea mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, huku akilazimisha
nyongeza ya mkataba utakaompa mshahara mkubwa wa pauni 130,000, lakini Man
United imekataa hilo
WASHIKA Bunduki wa jiji la London, Arsenal, wameripotiwa
kuratibu zoezi la kushtua la kusaka saini ya winga hatari raia wa Ureno
anayekipiga Manchester United, Luis Nani ambaye amebakisha kipindi kifupi cha
mkataba wake na anaweza kuondoka Old Trafford Janurai mwakani.
Arsenal imedaiwa kujiweka sawa na dau la pauni milioni 20,
ili kumtwaa Nani kama mbadala wa winga anayesuasuia kusaini nyongeza ya mkataba
klabuni Emirates, Theo Walcott, ambaye naye kama Mreno huyo, amebakisha kipindi
kifupi anachoapswa kukirefusha huku akidengua kufanya hivyo.
Ili kumuachia Nani, Man United inahitaji dau nono kuliko
lile la pauni milioni 14 ambalo iliilipa Sporting Lisbon mwaka 2007 kupata
saini ya winga huyo na bosi wa Arsenal, Arsene Wenger yu kikaangoni
akishinikizwa na bodi ya klabu pamoja na mashabiki kufanya usajili wa majina
makubwa kwa dau nono.
Nani, 26, kwa sasa yuko nje ya kikosi kutokana na matatizo
ya nyama za paja, akiwa na salio la mkataba wa miezi 18, ambao unamuwezesha
kupokea mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, huku akilazimisha nyongeza ya mkataba
utakaompa mshahara mkubwa wa pauni 130,000, lakini Man United imekataa
hilo.
Wakati Arsenal ikiwa tayari kumpa mkataba wenye mshahara wa
pauni 80,000 kwa wiki kwa winga wake Walcott, wameonesha kuwa wana uwezo na
utayari wa kulipa mshahara zaidi ya huo kwa wachezaji wengine. Andrey Arshavin
anapokea mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, kama ilivyo kwa Mjerumani Lukas
Podolski.
Klabu mbili zinazotumia zaidi pesa katika usajili barani
Ulaya za Zenit St Petersburg ya Russia na Paris St Germain ya Ufaransa,
zimetajwa kumwania Nani, Mreno anayependa kubaki katika Ligi Kuu ya England,
ambako pia matajiri wa jiji la London, Chelsea wanasikilizia mchakato wake Old
Trafford utaishaje.



Post a Comment