CHUO
cha Usafirishaji (NIT), kwa mara ya kwanza kinaanzisha mitaala mipya ya mafunzo
ya wataalamu wa uchukuzi na usafirishaji mbayo italisaidia taifa kuondokana na
uhaba wa wataalamu katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji
nchini.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salam jana, wakati wa mkutano wa kujadili uanzishwaji wa
mitaala hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho, alisema mafunzo ya wataalamu hao
yatakuwa ya ngazi ya shahada ya uzamili.
Alibainisha kuwa mitaala
hiyo itajihusisha katika kutoa na mafunzo kwa wataalamu haswa katika sekta ya
bandari, reli, barabara, upande viwanja vya ndege na maeneo mengine yanayohusu
usafirishaji.
Maganilwa alisema serikali
inakabiliwa na uhaba wa wataalamu hao, huku wachache waliopo kuamua kubobea
zaidi katika sekta ya viwanda.
Aidha, serikali imeamua
kuimarisha miundombinu ya reli baada ya kubaini kuwa ndiyo chachu ya maendeleo
hivyo inalazika kukifufua chuo cha watalamu Tabora ambacho walikitelekeza na
kutegemea waalamu zaidi kutoka Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA),
ambao nao sasa wamezeeka hivyo kuna ulazima wa chuo chetu kutoa mafunzo ya aina
hiyo kwa vijana wenye damu changa.
“Tukubali kuwa nchi
inapokuwa na miundombinu ya uhakika ni fursa ambayo inasaidia kuinua uchumi wa
nchi hivyo kuanzishwa kwa mafunzo ya wataalamu hao kutakuwa chachu kubwa ya
kutuletea mabadiliko katika usafirishaji”alisema
Maganilwa.
Maganilwa aliongeza kuwa
wataalamu hao ni muhimu katika sekta mbalimbali kwani uwepo wao utasaidia zaidi
katika kuliletea taifa hili maendeleo ambayo ndiyo kiu ya jamii.


Post a Comment