CHAMA Kuu cha Upinzani
nchini Ghana kimewasilisha kesi katika mahakama kuu zaidi nchini humo kupinga
ushindi wa rais John Mahama katika uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi
huu.
Chama cha National
Patriotic Party (NPP) kimepinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe Saba
Desemba, ikidai ulikumba na udanganyifu mkubwa.
Tume ya uchaguzi nchini
humo ilisema kuwa Bwana Mahakama alipata asilimia 50.7 ya kura zote zilizopigwa,
idadi ambayo ni kubwa na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mgombea
wa chama cha NPP Nana Akufo-Addo, ambaye alipata asilimia 47.7 ya
kura.
Waangalizi wa kimataifa
walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Chama hicho cha NPP,
kimesema imewasilisha kesi hiyo baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa vituo
elfu ishirini na sita vya kupigia kura, vilivyokujwa na zaidi ya kura milioni
kumi na moja.
Akufo-Addo alishindwa
katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2008, kwa asilimia moja lakini
alikubali matokeo hayo.
Bwna Mahama wa chama cha
National Democratic Congress party, alikuwa makamu wa rais wa Ghana hadi kifo
cha ghafla cha rais wa hiyo hiyo John Atta Mills, mwezi Julai mwaka huu, ambako
aliteuliwa kuhudumu kama kaimu rais wa nchi hiyo.
Taifa la Ghana
limekisiwa kuwa nchi iliyo na demokrasia iliyokomaa na thabiti zaidi barani
Afrika.
Post a Comment