WAZIRI wa Ujenzi, John
Magufuli amemteua Prof Ninatubu Lema kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia
(CoET), kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), uteuzi huo
unaanzia Desemba 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Magufuli iliyosambazwa kweye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, na
kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Herbet Mrango, ilieleza kuwa uteuzi huo,
utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu hadi Desemba 20, 2015.
Kwa mujibu wa sheria Na.
15 ya mwaka 1997 ya mabadiliko madogo ya sehemu ya 3(3) ya kifungu 1(1) (a), na
1(2), kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 24 ya mwaka 2007, ndiyo iliyomfanya
Waziri afanye uteuzi wa wajumbe wa Bodi hiyo akiwemo mwenyekiti
huyo.
Katika uteuzi huo,
Magufuli pia aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ya ERB, kuwa ni pamoja na
Fintan Kilowoko kutoka wizara hiyo, ambapo kwa sasa ni mkurugenzi wa Barabara za
Mikoa, Joseph Malongo, ambaye kwa sasa ni Msajili Msaidizi Huduma za Usajili na
Gemma Modu kutoka Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Nuberis Nyange
kutoka Chama cha Wahandisi Washauri nchini (ACET).
Wengine ni Sarah
Barahamoka, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edwin Ngonyani kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Prof Bakari Mwinyiwiwa; Mhandisi Mwandamizi, Chuo
cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Prof.
John Kandoro; Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam
(DIT).
Waziri alisema kuwa
jukumu la msingi la Bodi hiyo ya Usajili wa Wahandisi ni kusajili wahandisi
pamoja na Kampuni zinazotoa ushauri wa kihandisi, kuendeleza wahandisi
kitaaluma, kuwajengea uwezo wa Wahandisi wa kitanzania.
Pamoja na kuandaa
nakuchapisha makala mbalimbali yanayohusu shughuli za kihandisi
nchini.
Post a Comment