KIKOSI cha wachezaji 27
wa Yanga Sc kinatarajiwa kuondoka nchini usiku wa jumamosi kuelekea nchini
uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya kujiandaa na mashindano
mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya
Mashindano na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkleb amesema
maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na kwamba wachezaji watakaokwenda huko
pamoja na viongozi watajulikana kesho.
Amesema kwamba kambi
hiyo itakisaidia sana kikosi katika maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa ligi
kuu ya vodacom pamoja na michuano ya Kagame itakayofanyika Kigali, Rwanda ambapo
Yanga ni bingwa tetezi.
"Ndo maana tumetaka
kwenda Uturuki kwani huko kuna facilities nzuri kwa ajili ya kambi...pia huko
tunataraji kiucheza mechi kadhaa za kirafiki,"amesema.
Yanga inayonolewa na
Ernie Brandts jana ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker Fc
katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Post a Comment