WATU
watano wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti, ikiwemo ya ajali
ya gari ambayo ilisababisha kifo cha mmoja na kujeruhi wengine
watano.
Aidha mwingine amekutwa kando kando mwa Reli ya TAZARA akiwa amekufa huku mwili wake ukiwa na majeraha yanayodhaniwa alipigwa na kitu chenye ncha kali.
Kamanda
wa Polisi mkoani hapa Faustini Shilogile, alisema tukio la kwanza lilitokea
Desemba 12, mwaka huu saa 10 jioni eneo la Luvili Mtimbila Wilaya ya Ulanga,
Likihusisha gari kupata ajali na kusababisha kifo kwa Beatrice John (30) mkazi
wa Ifakara Wilayani Kilombero.
Aliwataja
waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa ni Gervas Salamba (49) mkazi wa Dar es
salaam, Sabrina Mlongile (45), Chrisi Kalvin (29) wakazi wa Ifakara Wilayani
Kilombero na Tetemula Madirisha (32), Sahan Madirisha wakazi wa Malinyi
Wilayani Ulanga,
Kamanda,
alisema majeruhi wote walitibiwa katika hospitali ya Lugala na kuruhusiwa, huku
mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali hiyo, ambapo chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari
hilo.
Alilitaja
gari hilo kuwa ni lenya namba za usajiri T 709 BTN aina ya Toyota Noah
iliyokuwa ikiendeshwa na Hassan Popo (49) mkazi wa Ifakara ikitokea Mtimbila
kuelekea Ifakara , na kwamba dereva huyo,a nashikiliwa atafikishwa mahakamani
mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Katika
tukio la pili Mwanaume mmoja, Matei Kitinde (45) mkazi wa kijiji cha Mambogi
alikutwa amefariki hatua 50 kutoka katika reli ya TAZARA huku mwili wake ukiwa
na majeraha kichwani, ubavuni na mkono wa kulia yanayoonesha kuwa alipigwa na
kitu chenye ncha kali.
Alisema
tukio hilo lilitokea Desemba 26 mwaka huu sa 2:30 asubuhi katika eneo la
Kiberege Tarafa ya Mang’ula Wilayani Kilombero na kwamba hakuna mtu yeyeote
aliyekamatwa kuhusika na mauaji hayo na polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini
waliohusika.
Akizungumzia
tukio la tatu alisema Mfanyakazi wa Mashamba ya Miwa ya umwagiliaji katika
Kiwanda cha Sukari Kilombero (ILLOVO) Gemson Kaduma (45) mkazi wa Kijiji cha
Msokwa aliktwa amefariki kwenye mashamba hayo Desemba 12 huku akiwa amelalaliwa
na mambomba ya kumwagilia miwa nakwamba uchunguzin unaendelea.
Katika
tukio la nne mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Masanja (37) mkazi wa
Ilonga Wilayani Kilosa amekutwa amefariki baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana
katika eneo la mashamba ya Mbegu ya Msimba Wilayani humo .
Alisema
tukio hilo lilitokea Desemba 24 mwaka huu saa 5 asubuhi katika mashamba hayo,
ambapo mikono ya marehemu huyo ilikutwa imefungwa kwa nyuma na kamba ya katani
huku sababu za kifo hicho zikielezwa kuwa zilitokana na kipigo kikali, na
kwamba uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na mauaji hayo.
Katika
tukio la tano alisema lilitokea Desemba 24 saa 1:30 usiku katika eneo la
Morogoro Hotel Manispaa ya Morogoro ambapo mtembea kwa miguu asiyefahamika
mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 45 hadi 55 alifariki dunia
papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki.
Hata
hivyo alisema mwili wa mwanaume huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro,nakwamba aligongwa na pikipiki
isiyofahamika namba iliyokuwa ikiendeshwa na Eliyopo Devid ambaye ni mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na mkazi wa Foresti Mjini
hapa.
Post a Comment