|
Maghala
ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya
yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya
uwanja wa ndege wa mwanjelwa |
|
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo |
|
Hakika
kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha
zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa
mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo
kubeba maji ya kuzimia moto |
|
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo |
|
Moja
ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo
akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kuokoa mali zake kwani moto
ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake |
|
Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto |
|
Kama kawaida kmufa kmufaana hapa vibaka wakigombea sahani na masufuria kwenye box |
|
Hakika
jeshi la polisi linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kuokoa mali za
wafanyabiashara ambao bidhaa zao zilikuwa katika maghala hayo hapa
polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia |
|
Kwakweli
ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa
baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa
limevunjwa kioo cha mbele |
|
Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo |
|
Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto |
|
Asubuhi hii moto ndiyo unaishia |
|
Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia |
|
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo |
|
Kamanda
wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari
leo amesema anawapongeza sana wakazi wa Mbeya hasa wale wa maendeo
yanayozunguka maghala yalioteketea kwa mtoto kwa ushirikiano wao
kuwezesha kuokoa baadhi ya bidha za wafayabiashara licha ya vijana
wachache kutaka kuiba na kutupa mawe askari wake ili wafanye uhalifu wa
kupora bidhaa zilizokuwa zinaokolewa hapo mpaka sasa vijana wawili
wamekamatwa kwa kutupiaaskari mawe na kuiba bidhaa zilizokuwa
zinaokolewa
chanzo: Mbeye Yetu
|
on Sunday, December 30, 2012
Post a Comment