Bila kujali mvua kubwa
inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la
Mboto.
Bila kujali mvua kubwa
inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi
rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo
la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13,
2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya serikali ya kujenga nyumba mpya 35
kwa ajili ya waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole,
Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume,
amejengewa nyumba ya vyumba vitano pamoja na fremu ya
duka.
Pichani juu na chini ni
Baadhi ya nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo
la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekana
leo Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.(PICHA
NA IKULU).


Post a Comment