TANZANIA
itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Vijana wa Kanda ya Afrika wa Jumuiya
ya Madola kuanzia Januari 28 hadi Februari Mosi mwaka huu.
Hayo yamesemwa (leo) na
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika ya Mpango wa Vijana wa Jumuia ya Madola, James
Odit wakati akizungumza na Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenella Mukangara kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
Mkurugenzi huyo alisema
mkutano utahusisha nchi 22 ambazo ni wanachama na jumla ya washiriki 60
wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kutoka katika wizara zinazohusiana na
masuala ya vijana, viogozi wa vijana, viongozi wawakilishi wa Baraza la Vijana,
wawakilishi wa kimataifa, viongozi wa kikanda wa maendeleo ya vijana na Jumuiya
ya Madola.
Miongoni mwa mambo mengine
waliyojadiliana ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Vijana na jinsi ya kuunda
Katiba ya Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola.
“Mkutano huu utajadili
namna ya kuunda Barazala Vijana la Jumuiya ya Madola(CYC) na program za
maendeleo ya vijana na jinsi ya kuwawezesha katika shughuli mbalimbali za
kimaendeleo,” alisema Odit.
Kwa Upande wake Waziri wa
wizara hiyo, Dk. Mukangara alisema anaishukuru jumuiya hiyo kwa kuichagua
Tanzania kuwa mwejeji wa mkutano huo. Huku akisema suala la uundaji wa Baraza la
Taifa la Vijana hivi sasa liko katika hatua ya ngazi za
juu.
Waziri huyo alizitaja
changamoto za kuendeleza mipago mbalimbali ya maendedeleo ya vijana kuwa ni
kukosefu wa fedha za kutosha mfano vile kuwawezesha vijana katika shughuli za
kiuchumi na kimaendeleo, kuwajengea uwezo, kuwapatia ajira, ujuzi na
elimu.
Akifafanua kuhusu suala
hilo Mkurugenzi huyo alisema atalifikisha suala hilo kwa wenzake ili waweze
kungalia namna ya kuweza kushirikiana.
Waziri Mukangara alishauri
jumuiya hiyo kuangalia namna ya kuweza kushirikiana katika maeneo mengine
ambayo ni sekta ya Michezo, Utamaduni na Habari.


Post a Comment