RAIS WA JAMUHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KESHO ANATARAJIWA
KUZINDUA RASMI MATOKEO YA AWALI YA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI.
SHEREHE ZA UZINDUZI HUO
UTAKAOAMBATANA NA KUTANGAZA KWA MATOKEO YA IDADI YA WATANZANIA ZITAFANYIKA
KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM NA ZITAHUDHURIWA NA
VIONGOZI MBALI MBALI WA KITAIFA NA WANANCHI.
KUTANGAZWA KWA MATOKEO
YA AWALI YA IDADI YA WATU,NI HATU YA MWANZO KATIKA UTARATIBU WA UTOAJI WA
TAKWIMU ZITOKANAZO NA SENSA YA WATU NA MAKAZI,AMBAPO MATOKEO MENGINE
YATAENDELEA KUTOLEWA KWA AWAMU.
OFISI YA TAIFA YA
TAKWIMU NA OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, INAWATAKA
WANANCHI,WANAHARAKATI NA WADAU WENGINE WOTE WA MAENDELEO KUTUMIA TAKWIMU HIZO
KWA UFANISI WA MAHITAJI YAO NA MAENDELEO YA TAIFA KWA UJUMLA.
ZOEZI LA SENSA YA WATU
NA MAKAZI LILIFANYIKA TANZANIA NZIMA KUANZIA TAREHE 26 AGOSTI HADI TAREHE 8
SEPTEMBA MWAKA HUU.
on Sunday, December 30, 2012
Post a Comment