CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaonya wafanyakazi wa Serikali wanaoshabikia vyama vya siasa kikiwataka kuacha kufanya hivyo.
Kauli hiyo ya CCM imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara), Mwigulu Nchemba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kibaha, mkoani Pwani.
Kiongozi huyo wa CCM alieleza kuwa wapo watumishi wa Serikali, ambao wanawafahamu hawatekelezi Ilani ya CCM inayowataka kuwatumikia wananchi, badala yake hutumia muda wa kazi kushabikia siasa, hasa vyama vya upinzani na kukwamisha nia njema ya CCM na Serikali yake.
Kiongozi huyo wa CCM alieleza kuwa wapo watumishi wa Serikali, ambao wanawafahamu hawatekelezi Ilani ya CCM inayowataka kuwatumikia wananchi, badala yake hutumia muda wa kazi kushabikia siasa, hasa vyama vya upinzani na kukwamisha nia njema ya CCM na Serikali yake.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Nchemba alisema kwamba watumishi hao walio katika kada mbalimbali wanarudisha nyuma maendeleo.
Alisema kuwa mtumishi wa umma lazima awe anayejali miiko na maadili ya kazi na kwamba kinyume na hivyo, anapaswa kujiondoa mwenyewe kazini.
“Umefika wakati wa kuchagua moja kama chama ni chama na kazi ni kazi. Kuanzia leo akionekana mtumishi wa umma, awe mwalimu au daktari hatavumiliwa,” alisema Nchemba akionya.
Aidha, Nchemba alisema pia kwamba CCM kinayumba kutokana na kuwa na makundi ya watu, ambayo yameweka masilahi binafsi mbele.
Alifafanua kuwa ubinafsi huo unakiweka chama hicho katika wakati mgumu huku akiwataka watu wanaotanguliza masiahi binafsi mbele kuacha tabia hiyo, badala yake watangulize masilahi ya chama mbele.
Akizungumzia michango mbalimbali inayotozwa na Serikali katika maeneo ya huduma, alisema kuwa michango hiyo ipo kisheria ili kuwezesha huduma husika kuwa endelevu na zenye ubora, ambapo aliwataka wananchi kuondokana na dhana kuwa kuchangia huduma hizo ni kuibiwa.
Post a Comment