Vilabu vya Uingereza vitaadhibiwa vikiwa vitapatikana na hatia
ya kutochukua hatua za kukabiliana na ubaguzi wa rangi miongoni mwa wachezaji,
makocha na mashabiki, chini ya sheria mpya ya shirikisho la mchezo wa soka
nchini Uingereza.
Katika mpango ambao unatarajiwa kuwasilishwa kwa serikali, shirikisho la FA
pia linatarajia kuwa na angalau asilimia kumi ya maafisa wakuu wa kiufundi na
marefa kutoka kwa watu wanaotoka kabila ndogo.Mpango huo umeafikiwa na vilabu vyote vya Uingereza, kufuatia mkutano ulioitishwa na ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Februari mwaka huu baada ya Luis Suarez na John Terry kutuhumiwa kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi.
Mpango huo umeidhinisha na FA, Ligi kuu ya Premier, Ligi Daraja ya kwanza, chama cha wachezaji wa kulipwa PFA na chama cha makocha wa ligi kuu LMA.
Mwenyekiti wa FA, David Bernstein amesema, huo ni dhihirisho ya kujitolea kwao, kwa niaba ya mchezo huo nchini Uingereza ili kuhakikisha kuwa hakuna visa vyovyote vya ubaguzi.
Ameongeza kusema kuwa juhudi hizo zitafanikiwa ikiwa wadau wote watashirikiana kuleta mabadiliko.
BBC
Post a Comment