Simba SC |
Na Ally
Mohamed, Zanzibar
MABINGWA wa
soka Tanzania Bara, Simba SC wamepangwa kundi moja, A na Tusker FC ya Kenya,
Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi,
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni visiwani
Zanzibar.
Aidha,
katika Kundi B, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, Azam FC ya Dar e Salaam
pia, imepangwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union ya Tanga na Miembeni
ya Unguja.
Michuano ya
Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu
ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka
49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka
ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu
wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano
hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi
itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka
kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho
Barani Afrika, pamabano litakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini
Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja
pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa
soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini
Kenya, Tusker.
Kwa mujibu
wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo
yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi
mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
Awali
michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini
kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na
klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani
Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1
januari.
Bingwa wa
michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh. Milioni kumi
(10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi
nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji
bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu
bora na zawadi nyeanginezo.
Post a Comment