SIKU moja baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Wiliam Mgimwa, kuwataka
wananchi wasiwe na wasiwasi licha ya deni la taifa kuzidi kuongezeka, Waziri
Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe na Profesa Ibrahim Lipumba, wamesema kauli hiyo
inatia mashaka.
Waziri Mgimwa juzi alikaririwa akiwaasa Watanzania kuwa pamoja na ukuaji wa deni hilo linalofikia sh trilioni 20 kwa sasa, wasiwe na wasiwasi kwani serikali imejikita katika kuboresha huduma za maji na umeme wa gesi kuanzia Mtwara kuja Dar es Salaam.
Hata hivyo wakati Mgimwa akieleza hayo, wataalamu wa uchumi wamehofia kasi ya deni hilo kuzidi kukua.
Akizungumza na gazeti hilo jana kwa njia ya simu, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema kuwa Watanznia wanapaswa kuwa na wasiwasi na deni hilo.
Zitto alirejea kauli yake aliyoitoa bungeni na kuitaka serikali ifanye ukaguzi maalumu kubaini uhalali wa deni hilo.
Alisema kuwa ukaguzi ukifanyika utawezesha kujulikana kama miradi iliyotekelezwa imefanyika kama inavyotakiwa au kuna mazingira yenye utata.
Zitto ambaye alishangazwa na kauli ya Mgimwa, alisisitiza kwamba wananchi wana haja ya kuwa na wasiwasi wala wasidanganywe na kauli hiyo.
Alifafanua kuwa mwaka 2007 baada ya msamaha, deni hilo lilifikia kiwango cha dola za Marekani bilioni 3, lakini wakati huu wa kuelekea mwishoni mwa mwaka huu, limefikia dola za Marekani bilioni 14 sawa na ukuaji wa asilimia 400.
“Waziri wa Fedha anaposema kuwa wamewekeza katika sekta ya gesi na maji, hili suala si kweli, kwani bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam serikali imewekeza si zaidi ya dola bilioni moja,” alisema.
Alisema uwekezaji huo hauna tija kwani baada ya miaka mitano mradi wa kusafirisha gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam utakuwa hauna maana,” alisema.
Zitto aliongeza kuwa ni kwa utaratibu huo wa kukuza deni la taifa ndio hujitokeza watu wachache wakajinufaisha kwa kuiba kwa kutumia deni hilo, na kwamba ndiyo maana mwaka huu zimetumika trilioni 1.9 kama riba tu kwa ajili ya kulipia deni hilo.
“Inasikitisha kuwa tunalipa zaidi kuliko tunavyotumia hata katika kujenga madaraja, shule au vitu vingine. Hatutaki deni liendelee kukua kwa ajili ya mikopo ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari ya kifahari,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye pia ni mchumi kitaaluma, Prof Lipumba, alisema kuwa miaka ya 80 deni lilikua kwa kasi hadi Tanzania ikashindwa kulipa.
Nchi ikaanza kuomba msamaha isamehewe deni, lakini msamaha wa madeni hayo ulitumika vibaya ukaleta migogoro na wizi kama wa EPA na mengine yanayofanana nayo.
Prof. Lipumba aliishauri serikali iache kukopa katika masoko ya biashara ya nje ambayo yana riba za juu bila sababu, kwani kwa kufanya vile kunaendelea kukuza deni la taifa.
Pia aliitaka serikali ipunguze kukopa, ikusanye kodi na iache kutoa misamaha mingi ya kodi na itumie vema fedha za wananchi.
Aliungana na Zitto akisema kwamba wananchi wana kila sababu ya kuwa na wasiwasi wanapoona deni la taifa linakua siku hadi siku na kuwataka wasiwe kimya kutokana na kauli ya Mgimwa.

Chanzo: Tanzania Daima
Post a Comment