Wafungaji wa mabao ya Stars leo, Kiemba kulia na Bocco kushoto wakipongezana |
Na Mahmoud
Zubeiry, Kampala
TANZANIA
Bara imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya afrika Mashariki na
kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuilaza Rwanda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa
Lugogo mjini hapa mchana huu.
Hadi
mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri
Kiemba, dakika mya 33 akiunganisha pasi ya Mwinyi Kazimoto aliyewapunguza
wachezaji wawili wa Rwanda kabla ya kutoa pasi
maridadi.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Mohamed El Fadil kutoka Sudan, mshambuliaji John
Raphael Bocco ‘Adebayor’ alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Rwanda na
aliwafanya waende kwenye vyumba vya kupumzikia wakiwa
hoi.
Katika hicho
kipindi cha kwanza, Rwanda walikosa bao la wazi dakika ya 12 baada ya krosi ya
Jean Claude Iranzi kuokolewa na beki Kevin Yondan kwa kichwa na dakika ya 19
Jean Baptiste Mugiraneza alipiga juu akiwa nje kidogo ya eneo la
hatari.
Stars pamoja
na kufunga bao hilo kipindi hicho cha kwanza, katika dakika ya 30 krosi nzuri ya
Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa na Bocco walishindwa kuiunganisha na
ikawapita wote.
Ngassa tena,
katika dakika ya 38 alipiga shuti kali kutoka wingi ya kushoto, lakini likaenda
nje sentimita chache.
Kipindi cha
pili,
Kipindi cha
pili Stars walirudi vizuri tena na kuendelea kucheza kwa kuonana, ingawa na
Rwanda nao waliendelea kucheza kwa bidii kutafuta bao la
kusawazisha.
Hata hivyo,
walikuwa ni Stars tena waliofanikiwa kupata bao la pili 53 baada ya John Bocco
kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Jean Claude Ndoli kufuatia shuti kali la Mwinyi
Kazimoto kutoka nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao
hilo, Rwanda walionekana kupagawa, lakini hawakusahau kushambulia lango la Stars
na dakika ya 86 Dadi Birori hakujali ameotea akasukuma mpira nyavuni, lakini
refa akakataa bao hilo.
Kwa ushindi
huo, Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia kesho kukutana naye
kwenye Nusu Fainali.
Stars; Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Amri Kiemba,
Salum Abubakar/Athumani Iddi dk51, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa
na John Bocco/Shaaban Nditi dk 85.
Rwanda; Jean
Claude Ndoli, Emery Basiyenge, Ismail Nshutimayamangara/Fabrice Twagizimana
dk19, Jimmy Mbaraga/Imran Nshiyimana dk67, Charles Tibingana/Barnabe Mbuyumbyi
dk61, Michel Rusheshangoga, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jean
Claude Iranzi, Dadi Birori na Tumaine Ntamuhanga.
Post a Comment