Kibao cha Shule ya Sekondari ya
Bungu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bungu, Dismas Kimweli akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni
*Imeandaliwa na Thehabari.com kwa ushirikiano na HakiElimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bungu, Dismas Kimweli akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni
Na Mwandishi wa
Thehabari.com, Korogwe
SUALA la kuwepo na
utata kwa baadhi ya wanafunzi kukwamishwa na fomu namba 9 ya Takwimu za Shule za
Msingi kwa mwanafunzi (TSM9) kufanya mitihani yao katika shule anuai za
sekondari limezua mvutano kati ya wazazi wa wanafunzi na walimu huku kila upande
ukitupa lawama kwa mwenzake.
Baadhi ya wanafunzi na
wazazi waliohojiwa wamedai uzembe upo kwa walimu ambao hutumia majina ya
wanafunzi wengine kuingiza wanafunzi kinyemela, jambo ambalo huzua utata baadaye
kwa mwanafunzi aliyeingia kwa njia hiyo anapokaribia kufanya mitihani
yake.
Uchunguzi uliofanywa
na mwandishi wa habari hizi wilayani Korogwe katika shule kadhaa za sekondari na
msingi umebaini kuwa wapo wanafunzi ambao wamezuiwa kufanya mtihani wa mwisho wa
kidato cha nne na ule wa kidato cha pili wa mchujo kutokana na hali kama hiyo ya
utata katika suala hilo la TSM9.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Bungu, Dismas Kimweli ambaye shule yake ilikuwa miongoni mwa shule
zilizolalamikiwa, akizungumza na mwandishi wa habari hizi alipinga kuwepo na
wanafunzi waliozuiliwa kufanya mitihani yao kutokana na utata wa fomu namba
9.
Mwalimu huyo alisema
idadi kubwa la wanafunzi ambao hukumbwa na matatizo kama hayo ni wanafunzi ambao
huingia shuleni kwa njia ya uhamisho huku wazazi wao wakiomba mwanafunzi
aendelee kusoma wakati utaratibu wa kufuatilia uhamisho
ukiendelea.
“Unakuta mzazi
anamleta mtoto kujiunga na shule yako akitokea shule nyingine na anaomba
aendelee kusoma wakati akiendelea kufuatilia uhamisho...lakini baadaye anakaa
kimya sasa mtoto anakuwa anaendelea na shule bila kuwa na uhamisho ambao
hujumuisha TSM9, ikifika kipindi cha mitihani hapo linakuwa tatizo na mzazi
anajifanya kasahau,” alisema.
“Sasa kama mtu
hajatimiza vitu kama hizi anarushaje lawama kwa walimu au shule...lakini
ikifikia hatua hii wapo ambao huwaeleza nao kuelewa na wapo ambao huwa na
mvutano kidogo,” aliongeza mwalimu huyo.
Akitoa ufafanuzi wa
suala hilo, Kaimu Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Shaban
Shemzighwa alikiri kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya wanafunzi kutokuwa na TSM9
hasa wa kidato cha pili lakini alidai waliruhusiwa kufanya mitihani yao na wao
kuwaagiza wakuu wa shule wanazotoka kuhakikisha wanawasilisha namba zao kwenye
vituo inakosahishiwa mitihani.
“Taarifa za malalamiko
zilitufikia na baadhi ya Shule za Sekondari ambazo wanafunzi walikuwa na
matatizo hayo ni Bungu, Patema, Mfundia na nyinginezo, hapa nipo nje ya kituo
cha kazi hivyo ni vigumu kutaja idadi na shule zote,” alisema Shemzighwa
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu.
Aidha akifafanua zaidi
alisema wanafunzi wengi waliokuwa na matatizo kama hayo wa kidato cha pili ni
wale waliohama kutoka shule moja kwenda nyingine, ambao hawakuja na TSM9 zao.
“…Hata hivyo waliruhusiwa kufanya mitihani na maelekezo tuliwapa wakuu wa shule
kuhakikisha wanapeleka namba za wanafunzi hao katika kituo cha kusaishia
mitihani ili waweze kutambuliwa kihalali vinginevyo hawawezi kutambulika,”
alisema ofisa huyo.
Alisema inaonekana
kuna baadhi ya walimu wakuu walipokea wanafunzi bila TSM9, hata hivyo
haikujulikana kama ni kwa njia ya kinyemela au matatizo ya uhamisho kwa
wanafunzi hao kutoka shule moja hadi nyingine. Hata hivyo licha ya kiongozi huyu
kuitaja Bungu kuwa miongoni mwa shule zilizotolewa tarifa kuwa na tatizo la fomu
namba 9, mkuu wa shule hiyo alipinga shule yake
kuwemo.
*Imeandaliwa na Thehabari.com kwa ushirikiano na HakiElimu
Post a Comment