Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Zahor
Kassim Mohamed EL-KHAROUSY kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi katika
Bahari Kuu.
Taarifa iliyotolewa na
kutiwa saini leo, Ijumaa, Desemba 7, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue inasema kuwa uteuzi wa Bwana El Kharousy ulianza Novemba 28, mwaka huu,
2012.
Kabla ya uteuzi wake,
Bwana Kharousy alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es
Salaam.
7 Desemba,
2012
Post a Comment