Jamii imeshauriwa
kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kabla na baada ya kula sambamba ba kuhifdhi
vinyesi sehemu stahiki ili kuweza kujikinga na maambukizi ya maradhi ya
kuharisha na kutapika.
Ushauri huo umetolewa
na Afisa wa Kitengo cha Kudhibiti,kuzuia na kufuatilia nyenendo za maradhi
kutoka Wizara ya Afya Ali Ahmada Ali katika Semina ya kuwajengea uelewa wa
maradhi ya maambukizi Wanahabari iliyofanyika Ukumbi wa Elimu mbadala Rahaleo
mjini Zanzibar.
Amesema maradhi ya
kuharisha bado yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar hivyo jamii
inapaswa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maaradhi hayo ya
kuambukiza.
Ali amesema utafiti
unaonesha kuwa kunawa Mikono kabla na baada ya kula kunapunguza uwezekano wa
kupata maambukizi ya maradhi ya kuharisha kwa Asilimia 40 na hivyo kuitaka jamii
isipuuzie tabia hiyo.
Hata hivyo amesema
Serikali imejipanga vyema kuhakikisha maradhi hao hayasambai kwa kutoa elimu
mbalimbali sambamba na kuendesha programu za dharura kwa jamii kupunguza maradhi
hayo.
Awali akitoa mada
katika Semina hiyo Afisa wa Kitengo cha Afya na Mazingira Forogo Mtande
amewataka Waandishi wa habari kusaidia kuelimisha jamii namna ya kujikinga na
Maradhi hayo.
Aidha amezitaja athari
zinaoweza kupatika kutokana na Ugonjwa wa kuharisha kuwa ni pamoja na kupunguza
uchumi wa familia na taifa kwa ujumla kutokana na kusababisha utegemezi kwa
waathirika.
Forogo ametaja athari
nyingine kuwa ni pamoja na kuigharimu Serikali kutokana na kutumia fedha nyingi
kwa matibabu na kudumaza sekta ya Elimu kutokana na maradhi hayo kushambulia
sana Watoto waliochini ya umri wa miaka saba.
Kwa upande wao
Wanahabari hao walikitaka kitengo hicho cha Afya kufanya programu za elimu kwa
jamii kila mwanzo wa msimu wa Mvua ili jamii iweze kupata tahadhari mapema kabla
ya maambukizi kuanza.
Pamoja na kuendelea kwa
maradhi ya kuharisha na kutapika Zanzibar taarifa za Wizara ya Afya zinasema
hakuna ugonjwa wa Kipindupindu ZanzĂbar tokea mwaka 2009 hadi sasa.
Post a Comment