Jumla ya nchi kumi
katika eneo la Maziwa makuu zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja litakalokuwa na
jumla ya askari 4,000 katika kukabiliana na ghasia na vita vya mara kwa mara
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Waziri wa Ulinzi wa DR
Congo, Dakta Crispus Kiyonga amethibitisha uundwaji wa jeshi hilo, akisema
litafanya kazi chini ya usimamizi wa Tanzania.
Mapigano ya hivi sasa
mashariki mwa Congo yalizuka mwezi Aprili mwaka huu wakati waasi wa M23
walipoliasi jeshi la nchi hiyo na kusababisha watu laki tano kuyakimbia makaazi
yao wakihofia usalama wao.
Wakati huohuo, viongozi
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika, SADC,
wameanza mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini
Tanzania.
Wameanza kwa kufanya
kikao cha Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA
chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri wa
Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe,
kikao hicho cha TROIKA kimewakutanisha marais Jakaya Kikwete, Hifikepunye
Phohamba wa Namibia na Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Amesema mara baada ya
kikao hicho cha TROIKA viongozi hao watajumuika na Rais Yoweri Museveni wa
Uganda ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kimataifa wa nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu, pamoja na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa
sasa SADC.
Viongozi hao kwa pamoja
watajadiliana kwa kina matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar
na Zimbabwe ambapo watawasilisha mapendekezo yao katika mkutano mkuu wa viongozi
wote 14 wa SADC utakaofanyika kesho.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment