TANZANIA inatarajiwa kuwa
mwenyeji wa mkutano wa Vijana wa Kanda ya Afrika wa Jumuiya ya Madola kuanzia
Januari 28 hadi Februari Mosi, mwakani.
Mkurugenzi
wa Kanda ya Afrika ya Mpango wa Vijana wa Jumuia ya Madola, James Odit,
aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa kizungumza na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kuhusu maandalizi
ya mkutano huo.
Mkurugenzi huyo, alisema
mkutano huo utahusisha nchi 22 ambazo ni wanachama na jumla ya washiriki 60
wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kutoka katika wizara zinazohusiana na
masuala ya vijana, viogozi wa vijana, viongozi wawakilishi wa Baraza la Vijana,
wawakilishi wa kimataifa, viongozi wa kikanda wa maendeleo ya vijana na Jumuiya
ya Madola.
Miongoni mwa mambo mengine
waliyojadiliana ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Vijana na jinsi ya kuunda
Katiba ya Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola.
“Mkutano huu utajadili namna
ya kuunda Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola (CYC), program za maendeleo ya
vijana na jinsi ya kuwawezesha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo,”
alisema Odit.
Kwa Upande wake Waziri wa
wizara hiyo, Dk. Mukangara alisema anaishukuru jumuiya hiyo kwa kuichagua
Tanzania kuwa mwejeji wa mkutano huo.
Hata hivyo, aliema suala la
uundaji wa Baraza la Taifa la Vijana hivi sasa liko katika hatua ya ngazi za
juu.
Dk. Mukangara alizitaja
baadhi ya changamoto za kuendeleza mipago mbalimbali ya maendedeleo ya vijana
kuwa ni pamoja na ukosefu wa fedha za kutosha, mfano kama vile kuwawezesha
vijana katika shughuli za kiuchumi na kimaendeleo, kuwajengea uwezo, kuwapatia
ajira, ujuzi na elimu.
Waziri Mukangara aliishauri
Jumuiya hiyo kuangalia namna ya kushirikiana katika maeneo mengine kama vile
sekta ya Michezo, Utamaduni na Habari.



Post a Comment