Naibu
mkurugenzi wa Idara ya Vijana Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na michezo
James Kajugusi(katikati)akifungua kongamano la wajasiriamali vijana la
siku tatu linalofanyika kwenye ukumbi wa Don Bosco vijana Upanga jiji Dar es
salaamAmbapo amesema vijana wengi wakiwa wajasiriamali nchi itazidi kuwa na
amani mshikamano na utulivu kwa sababu watatumia muda wao katika shughuli za
kujiongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.tuna ziomba taasisi za fedha
kuwapa kipaumbele vijana ambao wana elimu ya ujasiriamali kwa kuwapa mikopo
yenye masharti nafuu.
Hii ni kwa sababu ya utaalamu na ujuzi
walionao ni rahisi kwa vijana wajasiriamali kufanya marejesho ya mikopo
waliopewa.Aidha kwa kuwa watakuwa wamekidhi vigezo vya kisheria,usalama wa
bidhaa zao utakuwa mkubwa zaidi kuliko wale wanaofanya biashara kiholela na kwa
kubahatisha.(kushoto) ni Ofisa Uhusiano wa Benki ya NBC Eddie
Mhina.(kulia katikati)Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi isiyokuwa
ya Kiserikali inayojishughulisha na uendelezaji wa wajasiriamali vijana Tanzania
Bara( YESI) Bw. Denis Maira(wakwanza kuli)Bw.Hassan
Ngoma
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi
isiyokuwa ya Kiserikali inayojishughulisha na uendelezaji wa wajasiriamali
vijana Tanzania Bara( YESI) Bw. Denis Maira akifafanua jambo kwenye kongamano
hilo la wajasiriamali vijana
Wadau mbalimbali kutoka sekta za
ujasiriamali wakifuatilia kwa umakini hotuba iliokuwa ikitolewa na
Naibu mkurugenzi wa Idara ya Vijana Wizara ya Habari , Vijana ,
Utamaduni na michezo ,James Kajugusi
Post a Comment