MBUNGE wa Ubungo
(Chadema), John Mnyika ametoboa siri kuhusu usafiri wa treni ya masafa mafupi
jijini Dar es Salaam, akisema kuwa unaingizia hasara serikali kiasi cha sh
milioni 10 kila baada ya siku tano.
Kauli hiyo ilitolewa jijini
mwishoni mwa wiki na Mbunge huyo, wakati alipokuwa kwenye ziara ya kichama
katika Kata ya Saranga na Kimara.
Mnyika alisema pamoja
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe kujitapa kuwa huduma hiyo inakubalika
kwa wananchi, bado haina tija kwa serikali kutokana na hasara hiyo, inayotokana
na gharama za uwendeshaji kuwa kubwa.
Alisema mipango ya
uanzishwaji ya usafiri huo ilikuwa yaa kurupuka kwani haikuwa na maandlizi ya
kutosha haswa katika upande wa miuondombinu ambayo nayo ni sehemu inayoingiza
hasara.
“Ninazo nyaraka
zinazoonesha mpango mzima wa usafiri huu, ambazo zinaonyesha kuwa bado
haujaleta jitija ispokuwa hasara”alisema Mnyika.
Katika hatua nyingine
alizungumzia mabilioni ya fedha yaliyofichwa nchini Uswis, Mnyika alisema
serikali haipaswi kusubiri wahusika watajwe, kwani watu hao
wanafahamika.
Alisema kwani baadhi ya
watu waliyofanya hivyo ni miongoni mwa mafisadi waliyotajwa kwenye mkutano
uliyofanyika Septemba 15, 2007 kwenye viwanja vya Mwembe Yanga,
Temeke.
Mnyika aliitaka serikali ya
Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya Rais Kikwete, isifanye mzaha kuhusu
mabilioni hayo, bali ifanye uchunguzi wa kina na wa haraka kisha iwakamate na
kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi huo wakutorosha mabilioni
hayo.
Aidha, alitoa angalizo kuwa
endapo serikali hiyo ya CCM itashindwa kufanya hivyo basi atalizimika kupasua
bomu kwa kuwataja wahusika katika bunge lijalo.
Akizungumzia kuhusu kazi za
chama, Mnyika alisema kuwa alifanya mikutano 10 kwenye matawi ya kata hizo,
ambapo miongoni mwakazi hizo ilikuwa ni kutoa taarifa za utendaji wake wakazi
katika kupigania kero zinazo wakabili wananchi wa jimbo
hilo.
Pia alizindua vikundi vya
wajasiriamali ikiwemo Umoja wa Wanawake Mavurunza Kimaara (Women Group), ambapo
katika uzinduzi huo aliendesha harambee kwa ajili ya kutunisha mfuko wa umoja
huo.
Katika harambee hiyo,
Mnyika alichangia sh milioni 1, huku Wabunge wa Viti Maalumu Naomi Kaihula na
Joyce Limo wakichangia sh 500,000 kila mmoja huku jumla ya sh milioni 3.8
zikipatikana katika harambee hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Umoja
huo,Blandina Mrutu aliwashukuru viongozi hao, na kuahidi kuwa fedha hizo
zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa na umoja huo wenye wanachama
15.
Post a Comment