Mwalimu Nyerere akibebwa juu juu na Watanganyika waliokuwa na furaha baada ya kufanikisha Uhuru wa Tanganyika 1961 kutoka kwa Waingereza
Mwalimu Nyerere alisimikwa kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika. Kipindi hicho, Uwaziri Mkuu ndio kilikuwa cheo cha juu zaidi hatukuwa na cheo cha Urais
Mwalimu Nyerere akichanganya udongo wa Bara (Tanganyika) na Visiwani (Zanzibar) kuashiria kuundwa rasmi kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo ilikuwa mwaka 1964
Muungano wetu umepatikana kwa mambo makuu mawili. Kwanza, maridhiano baina ya pande mbili za Bara (Tanganyika) na Visiwani (Zanzibar) yaliyosimamiwa kikamilifu na Waasisi Hayati Nyerere na Hayati Karume; Pili Muungano wetu uliundwa kisheria zaidi kupitia makubaliano ya Hati za Muungano kama ambavyo Wanavyoonekana pichani waasisi wakibadilishana Hati za Muungano ambzo zilikuwa na makubaliano ya Mambo 11 (kipindi hicho)
Hii ni picha ya siku ya tukio la kuanzishwa kwa Azimio la Arusha mnamo 1967. Azimio la Arusha lilikuwa na lengo la kuondoa unyonyaji na matabaka ndani ya jamii zetu.
Mwalimu Nyerere alianzisha mbio za Mwenge kwa kuuwasha mwenge na kuwekwa juu ya Mlima Kilimanjaro ili uangaze kote ili penye chuki pawe na upendo; penye dhuluma pawe na haki n.k
Mwalimu Nyerere alifanikiwa vyema kujenga mahusiano mema baina ya Tanzania na nchi mbalimbali za Kiafrika na mataifa mbalimbali ya kimataifa.
Mwalimu Nyerere aliyaongoza majeshi ya Tanzania kwenye kuyaondoa majeshi ya Idd Amin yaliyovamia Kagera. Vita hiyo ilijulikana kama vita ya kagera iliyotokea mnamo 1978 na tulifanikiwa kuyaondoa majeshi ya Idd Amin.
Mwalimu Nyerere aliamua kung'atuka kwa hiari yake na kumuachia kwa njia ya kidemokrasia madaraka ya urais Alhaji Ali Hassan Mwinyi. Hiyo ilikuwa mnamo 1985.
Imeandaliwa na EMMANUEL JOHN SHILATU
on Sunday, December 9, 2012
Post a Comment