Nchi za Uganda na Sudan Kusini zimetiliana saini mkataba wa
kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na kuisalama ikiwa ni njia ya kuboresha
amani.
Makubaliano hayo ambayo
pia yamezungumzia kushirikiana katika Nyanja za fedha, biashara, utalii, elimu
na ushuru yametiwa saini jijini Kampala.
Waziri wa Nchi wa
masuala ya Kimataifa wa Uganda Okello Oryem ametia saini mkataba huo kwa niaba
ya serikali yake wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Nhial Deng Nhial
amesaini kwa niaba ya nchi yake.
Sudan Kusin imeshauriwa
kuomba kujiunga na Mamlaka ya Nile Basin, ambayo inazikutanisha pamoja nchi
zilizopo katika Nila Basin, ambapo chini ya ushirikiano na Uganda, pamoja na
mambo mengine nchi hizo mbili zitaweza kufanya mashauriano ya pamoja juu ya
mipaka na kuweka mipaka hiyo.
Post a Comment