Waziri wa Jinsia wa Rwanda,
Aloysia Inyumba amefariki, jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akiwa bado kijana
aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, Inyumba alishiriki
kikamilifu katika kuasisi chama cha Rwanda Patriotic Front (RPF) mnamo mwaka
1987.
Katika Harakati hizo akawa
Kamishna wa Fedha wakati wa mapinduzi ya RPF ambapo alipata uwezo wa kuweza
kukusanya na kutunza fedha kwaajili ya Mfuko huo wa Mageuzi.
Inyumba alijizolea umaarufu
mkubwa wakati wa kufanya manunuzi ya sare mpya za jeshi la RPF kutoka Ujerumani
Mshariki maarufu kama Mukotanyi .
Inyumba alishika wadhifa
huo wa Waziri wa Jinsia tangu baada ya vita 1994, na baade kuwa mbunge kwa miaka
8 na kurudi tena katika baraza la Mawaziri.
Wakati wa kuzanzishwa kwa
RPF akiwa pamoja na marehemu Meja Peter Bayingana , alifanya kazi kubwa ya
kumshawishi Kanali Alex Kanyarengwe kujiunga nao.
Marehemu Inyumba
atakumbukwa kuwa alisafiri hadi Tanzania kufuta Kanyarengwe ambaye baade alikuja
kuwa Mwenyekiti wa RPF, kufutia kifo cha Generali Fred
Rwigyema.
Hadi mauti yanamfika ,
Inyumba alikuwa ni mtu muhimu sana kwa Rais Paul Kagame kwani alikuwa ni mtu
mwenye ushawishi mkubwa katika siasa.
Kifo cha Inyumba si pigo tu
kwa RPF lakini pia ni pigo kwa wana Rwanda wote.
Inyumba alikuwa
akiheshimiwa sana katika uwanja wa siasa hata kwa wale walio poteza imani zao
kwa Kagame kama vile Generali Faustin Kayumba Nyamwasa.
Post a Comment