Wanachama wa UWF (Unity of Women Friends) wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza matembezi yao hisani ya kilometa
tano kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya
Tandika na Tabata sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao
wanatoka kwenye familia duni,matembezi hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki huku
mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth
Missokia (wa tatu kutoka kulia)..
Wanachama wa UWF (Unity of Women Friends) wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Tandika na Tabata
sekondari
Mgeni
rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia
akizungumza machache wakati wa hafla fupi ya kuchangisha fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa
shule ya Tandika na Tabata sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na
wengi wao wanatoka kwenye familia duni,Bi Elizabeth kupitia shirika hilo la
HakiElimu waliahidi kutoa shilingi milioni tatu ikiwa sehemu ya mchango wao
kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Mwenyekiti wa UWF (Unity of Women Friends),Esther Wakati
akifafanua madhumuni/lengo la matembezi hayo ya hisani kwa mgeni rasmi na wageni
waalikwa wengine,Easther alisema kuwa lengo la matembezi hayo ni kuchangisha
shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika wanafunzi
50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.
Mweka hazina wa UWF (Unity of Women Friends),Bi.Mwate Mwadinda
akitoa makusanyo yaliyopatikana kwenye matembezi hayo ya hisani ya Kilometa
tano,Mwate alisema kuwa hafla yao imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi
milioni kumi na laki mbili,hiyo ikiwa ni hatua ya awali ya muendelezo wa
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao
wanatoka kwenye familia duni
Meneja Mradi wa SOMKI (Somesha Mtoto wa Kike),Bi
Jane Magembe akizungumza machache mbele mgeni rasmi na wageni waalikwa
mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi,kuhusiana mradi/mfuko wa SOMKI
unatumika kuwasomesha watoto wa kike waishio katika mazingira magumu,Mradi huo
uko chini ya UWF.
Baadhi ya wanafunzi wanaosomeshwa na mfuko wa
SOMKI,kutoka kulia ni Khadija Hassan Chizenga anaesoma kidato cha nne shule ya
Sekomdari Kunduchi Girls High School pamoja na Ummilkhery Abdallah anaesoma
kidato cha sita shule ya sekondari Benjamin William Mkapa high
school.
Wanachama wa UWF wakifurahi
jambo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla
hiyo fupi iliyofanyika ndani ya Police Oficcers Mess,Oysterbay,jijini Dar
mwishoni mwa wiki.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,aitwae
Vumi akiimba kwa hisia mbele ya wageni waalikwa.
Pichani juu na chini ni wanachama wa UWF wakiwa
na mgeni rasmi sambamba na wageni waalikwa wakiwa kwenye matembezi ya hisani ya
kilometa tano,yakiwa na lengo ya kuchangisha
shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika wanafunzi
50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.Matembezi hayo yalidhaminiwa na
taasisi ya Foundation for Civil Society,kampuni ya Clouds Media
gROUP,Securix,ITRATECH LTD,Prime Time Promotions,Cool Blue pamoja na Equip
Davith Kahwa.
Post a Comment